June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ghorofa laporomoka Mwanza, watano wanusurika kifo

Jengo la ghorofa lililowahi kuanguka siku za nyuma jijini Dar es Salaam

Spread the love

UKUTA wa jengo la ghorofa saba linaloendelea kujengwa jijini Mwanza, umeporomoka na kujeruhi watu watano huku mmoja wao akivunjika mguu wakati wakiwa shimoni wakiendelea na ujenzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea leo saa sita mchana ni Rashind Khamis aliejeruhiwa mgongoni na mguuni, Benson Daud ambaye ni mahututi, Agustino Msindu, Ramadhan Hussein na Elias Bahati ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC).

Jengo hilo linalojengwa na kampuni ya Hyscon ya jijini hapa, ukuta wake umejengwa kando ya ukuta wenye ufa uliosababisha ajali hiyo.

Msaidizi wa msimamizi wa jengo hilo, William Samwel, amesema eneo ambalo limesababisha hitilafu hiyo walikuwa wameishali gundua  na  kwamba walikuwa wameishaanza kupatengeneza.
“Wafanyakazi hao walikuwa chini wakiendelea kurekebisha sehemu ambayo ilikuwa na hitilafu na pembeni ya eneo hilo pia kulikuwa na ukuta ambao ulikuwa na hitilafu ambao uliwaangukia,” amesema Samwel.

Mmoja wa majeruhi hao, aliyelazwa katika wodi ya dharura, Elias Bahati, akizungumza kwa taabu alisema alikuwa ndani ya shimo na wenzake wawili, ghafura alishituka kukuta ukuta uliojengwa kwa ajili ya kushikilia ukata unaojengwa ukiporomoka.

Alisema ukuta huo ambao umewajeruhi ulikuwa na hitilafu kubwa ikilinganishwa na hatua zilizochukuliwa na kwamba mmiliki alishindwa kuchukua hatua mapema ili kunusuru uhai wao.

 “Nimejeruhiwa vibaya sana, kama unavyoniona hapa, nimejeruhiwa kwenye mguu, kichwani na sehemu mbalimbali, yaani nakwambia ni Mungu katunusuru,” amesema.

Kiongozi wa wiki wa chumba cha dharura ambako majeruhi hao wamerazwa, Ernest Elesenguo, alithibitisha kupokelewa kwa majeruhi hao, na kwamba hadi sasa kuna mtu mmoja ambaye hajitambui.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, ambae aliwasili eneo la tukio akiwa ameambatana na kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo,Tito Mahinya, amsema amemuagiza Mkurugenzi kusitisha ujenzi wa jengo hilo licha ya kuwa mmiliki wake ana kibali cha ujenzi.

Konisaga amesema wamesitisha ujenzi ili kufanya tathmini upya na kufahamu namna ya kuweza kutatua suala hilo.

Mmiliki wa jengo hilo hakufahamika jina lake, licha ya kampuni yake kutambulika kama Mongo hardware iliyopo kitaru namba 6 barabara ya Nyerere jijini hapa.

error: Content is protected !!