July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ghasia za wafuasi wa Zuma zatia hasara Sh. 2.3 trilioni

Spread the love

 

GHASIA zilizoibuliwa na wafuasi wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, zimesababisha uharibifu wa mali zenye thamani ya Dola za Marekani 1 bilioni (Sh. 2.3 trilioni). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Ghasia hizo zilizotikisa kwa zaidi ya wiki moja, ziliibuka tarehe 8 Julai 2021, baada ya Zuma kujisalimisha gerezani, kwa ajili ya kutumikia kifungo cha miezi 15.

Adhabu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Kikatiba nchini humo, kwa kosa la kukaidi kuhudhuria kesi ya ufisadi inayomkabili mahakamani hapo.

Wakati wa ghasia hizo, wafuasi wa Zuma walivamia baadhi ya maduka na kuanza kupora bidhaa zilizomo ndani yake, pamoja na kuanza kuchoma moto majengo.

Mikoa iliyoathirika zaidi na ghasia hizo ni, Gauteng na KwaZulu-Natal.

Jana Jumapili, tarehe 18 Julai 2021, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametembelea Soweto katika Mkoa wa Gauteng, kwa ajili ya kukagua zoezi la usafi wa maeneo yaliyoathirika na ghasia hizo.

Rais Ramaphosa, aliwaomba wananchi wa nchi hiyo kuwa na umoja na mshikamano, badala ya kuendelea kufanya mizozo ya kibaguzi.

Alisema kwa sasa Serikali yake inafanya tathmini juu ya hasara zilizosababishwa na ghasia hizo.

Zuma anatuhumiwa kufanya ufisadi alipokuwa Rais wa Afrika Kusini, kuanzia 2009 hadi 2018.

error: Content is protected !!