Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Gharika Zimbawe, Msumbiji 120 wafariki
Kimataifa

Gharika Zimbawe, Msumbiji 120 wafariki

Spread the love

ZAIDI ya watu 120 wamepoteza maisha huku kadhaa wakipotea kusikojuliakana kutokana na kimbunga kilichotokea katika nchi ya Msumbiji na Zimbabwe. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kimbunga hicho kinachofahamika kwa jina la Ida, kilianzia nchini Msumbiji usiku wa Alhamisi tarehe 14 Machi 2019 na kusababisha vifo vya watu 62 na baadaye kiliingia nchini Zimbabwe na kuuwa watu 65.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amekatisha ziara yake huku Abu Dhabi kutokana na kimbunga hicho cha Ida.

Waziri wa Mazingira nchini Msumbiji, Celso Correia amesema kimbunga hicho ni janga kubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

Mbunge wa Chimanimani nchini Zimbabwe, Joshua Sacco amesema watu kati ya 150 hadi 200 wamepotea kusikojulikana na kwamba vikosi vya ukoaji vinaendelea na shughuli za kuokoa wahanga.

Jana Jumapili wanajeshi walisaidia shughuli za uokoaji na kufanikiwa kuwaokoa wanafunzi 200 walimu na watumishi kadhaa waliokwama katika shule moja iliyoko Chimanimani.

Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe umesema kimbunga cha Ida kimeatihiri watu takribani 10,000.

Hii ni mara ya pili kwa Zimbabwe kukumbwa na janga hilo, ambapo mwezi  Februari mwaka huu watu takribani 40 walifunikwa na vifusi katiika migodi nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!