July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gharama za vita dhidi ya IS kwa Uingereza

Moja aina ya bomu litakalotumika katika vita dhidi ya IS

Spread the love

BUNGE la Uingereza limeridhia mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la kigaidi lililoanzisha himaya inayodai kuwa ni Dola ya Kiislamu (IS). Makubaliano haya ya bunge la Uingereza yalipitishwa kwa kura 524 dhidi ya kura 43.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron alisema “Uingereza inapaswa kuunga mkono washirika wa kimataifa ili kuishambulia IS, jukumu ambalo ametoa tahadhari kwamba sio tu litachukua miezi bali miaka”

[pullquote]

Brimstone Precision Cruise

Urefu: 1.8m

Uzito: 50kgs

Gharama: 384 milioni

Storm Shadow Cruise

Gharama: 2,080 milioni

Tomahawk Cruise

Gharama: 780 milioni

Tornado GR4 aircraft

Gharama ya kusukwa: 91.2 milioni

[/pullquote]

Malcolm Chalmers, mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa masuala ya ulinzi na usalama (RUSI) alisema kwamba uhusika wa Uingereza kwa miezi saba katika vita ya kumuondoa Muamar Gadafi , kuelekea 2011 iliigharimu dola milioni 390 (Sh. bilioni 624 ) kama gharama za makombora na gharama za urushaji wa ndege.

Gharama hizo ni nyongeza ya bajeti ya ulinzi ya Uingereza ya mwaka uliopita inayojumuisha vifaa na malipo kwa wanajeshi iliyofikia dola bilioni 60, kiasi hiki ni sawa na bajeti ya Serikali ya Tanzania kwa miaka mitano na nusu.

 

Makombora maalumu

Siku ya Ijumaa iliyopita wakati Cameron akishawishi bunge alisema kuwa Uingereza ina hazina pekeee ya vifaa vya kijeshi, hazina ambayo hamna nchi washirika inaweza kutoa.

Cameron alitaja moja ya makombora yenye usahihi yanayoitwa Brimstone precision missile ambayo ni rafiki kwa raia kwani yakipigwa yanapunguza madhara kwa wananchi. Kombora hili linaweza kutolewa na Uingereza tu, alisema.

Makombora haya yanaweza yakalenga msafara pamoja na kundi la msafara wa vifaa unaoenda kasi. Mashambulizi ya aina haya hayakuwezekana siku za nyuma, haya yalisemwa na mchambuzi wa vifaa vya kivita, Ben Goodlad.

Brimstone linalosafari kwa kasi kubwa lina urefu wa mita 1.8 na lina uzito chini ya kilo 50. Kombora hili linaongozwa na rada kulekea kwenye shabaha yake na hivyo halihitaji rubani kulifyatua. Kombora hili linagharimu dola 240,000 (Sh. Milioni 384).

Kombora linginje litakalotumikaa linaitwa Storm Shadow Cruise lina thamani ya dola milioni 1.3 (Sh.2,080,000,000 ) na Tomahawk cruise kombora linalorushwa kwa kutumia Nyambizi linagharimu dola milioni 1.3 (Sh.milioni 780), hili linatumika maeneo ambayo ndege haiwezi kufika mfano maeneo yenye ulinzi mkali.

Marekani imekuwa ikitumia makombora ya Tomahawk kwa mashambulizi ya angani huko Syria tangu mwanzoni mwa wiki iliyopita, ikiwa imedondosha makombora aina hiyo 47 siku ya jumatatu iliyopita.

Kombora la Brimstone linarushwa na ndege za Tonado (Tornado GR4 aircraft). Ndege hizi zilitumika mwezi mmoja uliopita huko Iraq kutoa misaada ya kibinadamu. Sita ya ndege hizi tayari zipo kwenye kituo ya kijeshi cha Uingereza huko Cyprus. Kati ya ndege hizi mbili zilishaenda Iraq kutokea Cyprus na zimerudi salama.

Ndege hizo mbili hazikwenda kwa lengo la kufanya mashambulizi bali kwa lengo la kufanya upepelezi ili kubaini maeneo ya kushambulia.

Gharama za kurusha ndege ya Tonado inafikia Dola 57,000 (Sh. Milioni 91.2 ) kwa saa moja, hii ni kwa mujibu wa bunge la Uingereza lililokuwa linajadili shambulio dhidi ya Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi mwaka 2011. Ndege hizi zilizopo kwenye kituo cha jeshi cha Cyprus zin auwezo wa kuruka kwenda Iraq kwa muda wa saa moja tu.

Kuanzia Agosti 18 mpaka Septemba 23 Marekani imefanya mashambulizi ya angani 20 huko Syria na 198 huko Iraq.

error: Content is protected !!