January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gharama za maji zapanda Mwanza

Spread the love

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA) Mkoa wa Mwanza imeongeza bei ya maji kutokana na kupanda kwa gharama ya manunuzi ya mita za maji kuongezeka kufikia Sh. 1,075.74. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga wakati wa mkutano (Taftishi) uliohusisha Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Ewura (EWURA CCC).

Sanga amesema kuwa kutokana na kupanda kwa gharama za mita za maji kufikia kiasi cha Sh. 669.00 kimesababisha kuongezeka kwa bei ya maji, kwa watumiaji wa nyumbani na taasisi mbalimbali kufikia wastani wa Sh. 1,625.00 hivi sasa.

“MWAUWASA ili kufikia malengo yake na kuwa mamlaka bora Afrika Mashariki kwa kutoa huduma bora ya maji safi na salama na usafi wa mazingira Jiji la Mwanza, inapaswa kutolewa huduma kwa gharama stahiki na hiyo itatokana na mapato ya uhakika.

“Bei ya maji hazitakuwa chini ya gharama ya mita moja ya ujazo kama ilivyo sasa na hiyo itaenda sambamba na uboreshaji wa vifaa pamoja na miundombinu iliyochakaa,” amesema Sanga.

Sanga amesema wananchi wataweza kuboreshewa huduma kwa wateja, uboreshaji wa uzalishaji na usambazaji wa maji, uboreshaji na uondoaji na usafishaji wa majitaka pamoja na kurejesha gharama zote za huduma ya maji.

Kaimu Mwenyekiti Taifa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Ewura (EWURA CCC), Thomas Mkunguli amesema licha ya MWAUWASA kulalamikia upotevu wa maji, madeni makubwa na gharama ya manunuzi, tatizo hilo linatokana na mianya mikubwa ya upotevu wa mapato.

Hata hivyo amesema maeneo hayo matatu ya udhaifu yapo chini ya MWAUWASA na kwamba inaweza kuyadhibiti na kurekebishwa na yakaleta ongezeko la mapato pasipo kuongeza bei za huduma.

error: Content is protected !!