May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gharama kipimo cha corona Z’bar yapaa

Spread the love

 

KUPIMA virusi vya corona (COVID-19), visiwani Zanzibar sasa ni Dola za Marekani 80 (zaidi ya Sh.180,00), badala ya Sh.30,000 za awali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya afya visiwani humo jana Jumapili tarehe 28 Februari 2021, imeeleza bei hiyo mpya itakuwa kwa watu wote bila kutenganisha raia kutoka mataifa ya nje na wale wa ndani ya nchi.

Gharama za awali za kipimo hicho Zanzibar kwa wageni kutoka bje ya Afrika ilikuwa Dola za Marekani 80, wageni kutoka Afrika Mashariki 45,000 na raia wa visiwa hivyo Sh. 30,000.

Taarifa ya wizara hiyo inaeleza, msafiri yeyote atatakiwa kupima siku tatu kabla ya kusafiri kama ambavyo utaratibu wa awali ulivyokuwa.

Wizara hiyo imeelekeza hospitali zitakazotoa huduma hiyo ni pamoja na Migombani, Lumumba, Hospitali ya Blobal, Unguja. Pemba ina kituo kimoja ambacho ni Mfikiwa.

error: Content is protected !!