Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko GGML yatoa milioni 100 kudhibiti fisi wanaovamia wagonjwa Kasamwa
Habari Mchanganyiko

GGML yatoa milioni 100 kudhibiti fisi wanaovamia wagonjwa Kasamwa

Spread the love

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetumia jumla ya Sh milioni 100 kujenga uzio katika kituo cha afya cha Kasamwa kilichopo mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uzio huo umetajwa kuwa mwarobaini wa usalama wa kituo hicho cha afya ambacho nyakati za usiku kilikuwa kikikabiliwa na changamoto ya kutembelewa na wanyama wakali wakiwemo fisi waliokuwa tishio kwa wagonjwa na wahudumu wa afya kituoni hapo.

Akizungumzia msaada huo uliotolewa jana Makamu Rais wa AngloGold Ashanti anayeshughulikia miradi endelevu kwa nchi za Tanzania na Ghana, Simon Shayo alisema fedha hizo ni muendelezo wa jitihada za kampuni ya GGML kuboresha huduma za afya Mkoani Geita.

Alisema uboreshaji wa uzio katika kituo hicho cha afya ni muhimu katika kuboresha mazingira ya afya kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa GGML.

“Lengo la tatu la maendeleo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa linasisitiza kuweka mazingira bora ya afya na ustawi wa jamii yetu ifikapo mwaka 2030. Kampuni yetu ya GGML ingependa kuona huduma bora za afya zinaboreshwa katika kituo cha afya cha Kasamwa ikiwemo kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama wanaojifungua,” alisema Shayo.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Kasamwa Dk Thomas Mafuru ameishukuru kampuni ya GGML kwa kugharamia ujenzi wa uzio katika kituo hicho cha afya kwa sababu utazuia wanyama wakali nyakati za usiku na kurahisisha kazi ya walinzi kulinda rasilimali zilizopo katika kituo hicho.

“Tangu tuanzishe kituo cha afya Kasamwa kilichopo katika Halmashauri ya Mji Geita mwaka 2007, tumekuwa tukishirikiana vyema na kampuni ya GGML ambao wamekuwa pia wakitusaidia vifaa mbalimbali vikiwemo vitanda na magodoro,” alisema Dk. Mafuru.

Naye mkazi wa Kata ya Kasamwa Bi Susana Balele amepongeza ujenzi wa uzio huo kwa kuwa utawasaidia kuwa na amani nyakati za usiku wanapoleta wagonjwa katika kituo hicho cha afya.

“Nashukuru sana ujenzi wa huu uzio pamoja na kituo chote cha afya Kasamwa. Huduma zake ni nzuri na kwa sasa hatulazimiki tena kusafiri umbali mrefu hadi Geita mjini kwa ajili ya kupata huduma za afya,” alisema Susana.

GGML imekuwa kinara wa uwekezaji kwenye jamii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 ambapo vipaumbele vikuu vimekuwa ni miradi ya afya, elimu, maji, barabara, miradi ya kukuza kipato na miradi mingine mingi ya kijamii ili kuhakikisha jamii mwenyeji inapata maisha bora.

Mapema mwaka huu, GGML iliibuka mshindi wa jumla katika kampuni zinazofanya vizuri kwenye sekta ya madini nchini Tanzania kwa mwaka 2020/2021 baada ya kunyakua tuzo katika vipengele vya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, mazingira, usalama, mlipaji bora wa mapato (kodi) na uendelezaji wazawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!