September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

GGML yatoa mafunzo ya Covid-19 kwa waandishi wa habari 60 

Spread the love

KAMPUNI  ya uchimbaji wa Madini ya Dhahabu mkoani Geita (GGML) kwa kushirikiana na Ofisiya Mkuu wa Mkoa huo, imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari 60 wa Geita ilikuwajengea uelewa kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Mafunzohayo yaliyotolewa jana Mjini Geita,  piayamelenga kuwakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa chanjo ya Corona.

Akifunguamafunzo hayo, Makamu wa Rais wa GGML anayesimamia miradi endelevu ya kampuni, SimonShayo amesema GGML mbali na kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia fedhaza kudhibiti ugonjwa huo, imeona ni vema kufadhili mafunzo hayo ili kuwajengeauelewa wa kutosha waandishi wa habari.

Alisemamoja ya jukumu la kampuni ni kuhakikisha jamii zinazoizunguka zinanufaikakutokana na uwepo wa GGML mahala hapa.

“Kwahivyo, tumeamua kutumia mikakati tofauti kuendesha kampeni za uhamasishajinamna ya kujikinga na janga la UVIKO-19 na tumeungana na mikakati mbalimbali yaSerikali kuhamasisha watu wengi kuzingatia hatua, vigezo na taratibuzinazotolewa na watalaam wa afya wa Serikali ikiwamo umuhimu wa kupata chanjo.

“Nasemahivi kwa sababu chanjo hizi zina ufanisi mkubwa, na ni muhimu zaidi kwa sababukinga ni bora kuliko tiba. Kwa kujilinda sisi wenyewe, tunapunguza athari kubwaya UVIKO-19 kwa wale wanaotuzunguka. Tumeshuhudia mfano bora ukionyeshwa naviongozi wetu wakuu Kitaifa na hata Kimkoa na Kiwilaya kwa kuchanja hadharaniili kuwapa moyo wananchi wengine wachukue hatua ya kuchanja,” alisema.

Aidha,alisema kama sehemu ya ushirki wake kuunga mkono juhudi za Serikali, GGMLilitoa jumla ya Sh bilioni 1.6 kusaidia juhudi za kupunguza kasi ya kuenea kwaUVIKO-19. Lakini pia masharti na taratibu zilizokuwa zinafuatwa na GGML,zilizingatia miongozo iliyotolewa na Serikali ya Tanzania.

“Kati yafedha zote zilizotolewa, GGML ilitoa takriban Sh bilioni 1.1 kuchangia mfuko wakitaifa wa dharura katika kupambana na UVIKO-19. Mfuko huu ulioanzishwa naSerikali ulikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Jumlaya Shilingi milioni 500 zilizobaki zilitumika kusaidia mahitaji mbalimbali yamkoa na jamii inayotuzunguka hapa Geita hii ikiwa ni pamoja na utoaji wa vifaatiba na dawa muhimu vikiwemo vya kujikinga kwa watabibu, mitungi ya gesi nakadhalika,” alisema.

Aidha, JimmMtabwa aliyewakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wa Geita alitoa wito kwa waandishiwa habari kuungana na serikali katika kuelimisha wananchi kuhusu ugonjwa huo.

Wakati Katibu Mtendaji wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani, Geita, Novatus Lyaruumbali na kuishukuru GGML kwa mafunzo hayo, pia mafunzo hayo yatawasaidia kupatamajawabu ya maswali mengine yaliyokuwa yameibuka kuhusu chanjo ya Johnson&Johnson.

error: Content is protected !!