Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko GGML kujenga bustani ya kisasa Geita
Habari Mchanganyiko

GGML kujenga bustani ya kisasa Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akimuonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Richard Jordinson mchoro wa bustani ya kisasa itakayojengwa Geita Mjini, mwiingine ni Meneja Mahusiano wa GGML Joseph Mangilima
Spread the love

WAKAZI wa Mji wa Geita wanafurahia kuwa sehemu ya mradi wa bustani ya kupumzikia inayoanza kujengwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mradi huo uliotengewa bajeti ya Sh.70 milioni kutoka fedha za mfuko wa GGML za uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) zinatarajiwa kukamilisha mradi huo kabla ya mwisho wa mwaka 2020.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua ujenzi wa bustani hiyo katika kata ya Kalangalala mjini Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Gabriela.

Amesema, GGML kwa kushirikiana na Halmashauri ya Geita Mji inatekeleza mradi huo kupitia fedha CSR kutoka GGML.

Amesema mradi huo unaotekelezwa katika eneo la mita za mraba 4,000 katika kata ya Kalangalala mjini Geita, una lengo la kuwapatia wakazi wa Mji wa Geita fursa ya kuwa na eneo la kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kupumzika, kupunga upepo pamoja na kuepuka kero za joto.

“Lengo letu ni kuona wakazi wa Mji wa Geita wanafika katika eneo hili kufurahia upepo asilia sanjari na kuona mnara maalum wenye kumbukumbu ya Mkoa wa Geita.

“Bustani hii itakuwa kivutio pia kwa vile inajengwa kwa tofali za kuvutia kwenye maeneo yote ya kupitia na sehemu za watu kuketi hali ambayo itashawishi watu wengi zaidi kukaa na kujionea uzuri wa Mji wetu wa Geita,” amesema Gabriel.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson amesema kampuni ya GGML imekuwa ikifanya jitihada kubwa kubadilisha muonekano wa jamii ya Mkoa wa Geita kwa kuanzisha miradi endelevu.

“GGML tunajivunia kuwa, wakati tunasherehekea miaka 20 ya uwekezaji wetu ndani ya Mkoa wa Geita mwaka huu, tumefanikiwa kutekeleza miradi mingi yenye tija na matokeo chanya ikiwemo mnara wa makutano ya barabara Mjini Geita, masoko, taa za barabarani, vituo vya afya, shule na barabara za lami,” amesema Jordinson.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!