Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko GF Truck yawatangazia neema wakandarasi wadogo
Habari Mchanganyiko

GF Truck yawatangazia neema wakandarasi wadogo

Spread the love

 

KAMPUNI ya GF Trucks & Equipmentís imepanga kuanza kuwakopesha vitendea kazi wakandarasi ili kuhakikisha wakandarasi wadogo na wakati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Lengo ni kuwakomboa na hali mbaya ya kuchelewesha miradi mbalimbali wanayopatiwa.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi tarehe 12 Mei 2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuzaji wa Magari (trucks) na Mitambo ya Kutengenezea Barabara wa GF Trucks & Equipmentís Ltd, Salman Karmal katika mkutano wa Bodi ya Wakandarasi Tanzania.

Karmal amewataka wakandarasi na wahandisi nchini kununa magari na mitambo katika kampuni hiyo kwani wanautaratibu mzuri wa kuwakopesha wakandarasi wadogo na wakati ambao wana miradi tayari.

Amesema GF wanakitengo maalumu kwa kushirikiana na taasisi za kibenki ili kumwezesha mkandarasi kupata mitambo na magari kwa masharti nafuu.

Kampuni hiyo inayojishungulisha na uuzaji wa Magari ya FAW, HONG YANG na mitambo aina ya XCMG.

Mmoja wa wanufaika wa mpango huo wa kampuni hiyo ambaye amefaidika na huduma hiyo ya kukopeshwa vitendea kazi, Mhandisi Baraka Emanueli amesema, kupitia kampuni hiyo walianza na Tipper moja na sasa wanamiliki magari matatu walioanza kukopa miaka mitatu iliyopita.

Amesema wamefanikiwa kulipa na hatimaye kwa sasa wamechukua mashine ya XCMG hivyo utaratibu huo umewanufaisha wao ambapo wanapata zabuni za kuchukua makaa ya mawe ambayo awali hawakuwa na uwezo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!