Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa George Weah afanya kweli Liberia, aibuka mshindi urais
Kimataifa

George Weah afanya kweli Liberia, aibuka mshindi urais

George Weah, Mshindi wa Urais
Spread the love

ALIYEWAHI kuwa mchezaji bora wa dunia, Georgr Weah ameibuka mshindi wa kiti cha urais nchini Liberia katika uchaguzi uliofanyika juzi.

Weah amewahi kuichezea timu za Monaco, Mancity na Chelsea, ameshinda uchaguzi huo ambao ulikuwa na ushindani mkali.

Katika uchaguzi huo, Mwanamama Ellen Sirlif ambaye ni rais wa sasa hakugombea kutokana na matakwa ya katiba ya nchi hiyo ambayo inazmuia kugombea kiti hicho zaidi ya vipindi viwili.

Ellen aliingia Ikulu mwaka 2006 na sasa Weah, mchezaji bora wa dunia wa zamani ambae uchezaji wake ulitokana na mchango wake kwa club yake zamani anatarajia kula kiapo kuongoza nchi hiyo.

Weah alisajiliwa Monaco AS na kocha wa sasa wa Arsean Fc, Arsene Wenge. Uchaguzi wa 2006 uliompa ushindi Ellen, Weah aligombea na aliungwa mkono na Wenger.

Huyu ndiye George Weah wa Liberia
George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah ni mwanakandanda mashuhuri duniani na mwanasiasa aliyegombea urais wa Liberia mwaka 2005.

Weah alizaliwa 1 Oktoba 1966 katika jiji la Monrovia alikuwa na alikulia katika kitongoji cha masikini cha Clara. Kabla ya kujiunga na soka la kulipwa Weah alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Liberia kama fundi simu.

Kielimu, Weah ana Shahada ya Kwanza ya Uendeshaji Michezo toka Chuo Kikuu cha Parkwood, Londo, Uingereza. Mwaka 1999 alipata shahada ya Udakitari ya Heshima toka Chuo Kikuu cha A.M.E Zion nchini Liberia.

Mwaka 1995 Weah alipewa tuzo na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa Mwanasoka Bora Duniani. Yeye ni mwanasoka pekee toka Afrika aliyewahi kupewa tuzo hiyo.

Mwaka huo huo alichaguliwa pia kuwa Mwanasoka Bora Ulaya na Mwanasoka Bora Afrika.

Weah alianza safari yake ya soka katika timu ya Liberia ya Incincible Eleven na Tonnerre Yaounde, ya Cameroon.
Baada ya hapo alikwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya mwaka 1988.

Alijiunga na timu ya Monaco ambapo aliiongoza kushinda kombe la Ufaransa mwaka 1991. Baadaye alijiunga na [[Paris Saint Germain mwaka 1992-95.

Aliiongoza timu hii kuchukua kombe la ligi ya Ufaransa mwaka 1994. Mwaka 1995-2000 alikuwa akiichezea timu ya AC Milan ambayo ilishinda ligi ya Italia mwaka 1996 na 1999. Mwaka 2000 aliondoka AC Milan na kujiunga na Chelsea, baada ya muda mfupi alijiungana Manchester City na baadaye Marseille mwaka 2001.

Alimaliza soka la kulipwa akiwa na timu ya Al JAzira ya Falme ya Nchi za Kiarabu.

Weah amekuwa akitoa misaada kusaidia wananchi wa Liberia. Mwaka 2004 alipewa tuzo ya Arthur Ashe kwa juhudi zake za kusaidia kujenga nchi yake.

Kwa sasa Weah ameibuka mshindi wa kiti cha urais nchini Liberia ambaye sasa anasubiri kuapishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!