August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Geita yapata Askofu mpya

Spread the love

BABA mtakatifu Francis amemteua Padre Flavian Kasalla kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Geita, anaandika Wolfram Mwalongo.

Taarifa ya Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, iliyosainiwa na Padre Raymond Saba Katibu Mkuu wa wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imethibitisha uteuzi huo.

Kabla ya uteuzi huo Askofu Mteule alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris, Mtwara.

Padre Flavian Kasalla
Padre Flavian Kasalla

Kassala anakuwa Askofu wa tatu wa Jimbo hilo tangu lilipoanzishwa mwishoni mwa mwaka 1984, na Baba Mtakatifu Mwenyeheri Yohane wa Pili ambapo alimteua Aloysius Balina kuwa Askofu wa kwanza aliyedumu hadi Novemba mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa Askofu wa Shinyanga.

Askofu wa pili alikuwa ni Damian Dallu, aliyeongoza tangu mwaka 2000 hadi 2014 alipoteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Songea. Kati ya kipindi cha 1997 hadi 2000 kabla ya uteuzi huo Jimbo lilikuwa chini ya Msimamizi wa kipapa.

error: Content is protected !!