May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gazeti la Uhuru lasimamisha uzalishaji, vigogo 3

Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza kulifungia kwa siku saba Gazeti lake la Uhuru kuanzia leo Jumatano, tarehe 11 Agosti 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya gazeti hilo kukiri kuandika habari ya kupotosha juu ya mahojiano yaliyofanywa baina ya Rais Samian a Shirika la Utangaaji la Uingereza (BBC), tarehe 9 Agosti 2021, Ikulu ya Dar es Salaam.

Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi, liliandika habari kubwa leo Jumatano kwamba, “Sina wazo kuwania urais 2025” habari ambayo imeibua mjadala hasa ikizimngatiwa, katika mahojiano ya BBC hayakuoneshwa aliposema.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam amesema “kwa mamlaka yangu kama katibu mkuu, nimesimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba.”

Kabla ya kutangaza uamuzi huo, Chongolo amewaeleza waandishi wa habari kwamba, asubuhi ya leo, aliagiza Bodi ya Wakurugenzi ikutane na baada ya kukutana, imewasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji, Ernest Sungura, Mhariri Mtendaji, Athuman Mbutuka na Rashid Zahoro, ambaye alikuwa msimamizi wa gazeti hilo.

“Hawa walionekana kuhusika mojamoja kwenye usimamizi. Nimeipongeza bodi kwa uamuzi waliouchukua kwani uko ndani ya mamlaka yao,” amesema.

“Tunamwomba sana radhi Rais kwa kumlisha maneno, ukifuatilia mahojiano yoooote BBC hakuna sehemu amezungumza na muungwana ni vitendo. Tunamwomba radhi,” amesema Chongolo.

Tayari bodi imewasimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji, Ernest Sungura, Mhariri mtendaji na Rashid Zahoro ambaye yeye alikuwa msimamizi wa gazeti pamoja na kuunda tume ya kuchunguza nini hasa kilitokea- Daniel Chongolo, Katibu Mkuu CCM

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametangaza kusimamisha uchapwaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba kuanzia leo Jumatano kwa kuandika habari ya kupotosha juu ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan “tunamwomba radhi sana Rais kwa kumlisha maneno.”

error: Content is protected !!