
MASHAMBULIZI ya Jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza, Palestina yamesababisha vifo vya wapalestina 179, wakiwemo watoto 40 katika siku tano mfukulizo. Inaripoti Aljazeera…(endelea).
Raia wa Palestina wamekuwa na kazi ya kubeba miili ya wenzao waliouawa pia waliojeruhiwa katika fujo zinazoshika kasi Gaza.
Miongoni mwa picha zilizosambaa kwa kasi kubwa na kuibua hisia kali, ni wakati raia wa Palestina wakitoa ndani jeneza la Mahmud Tolba (15), aliyeuawa kwa makombora ya Israel usiku wa kuamkia jana tarehe 14 Mei 2021.
Mahmud alikuwa miongoni mwa waombolezaji katika msiba wa ndugu yao Haithan Imad uliotokea kwenye mji wa Al Zaitun, Mashariki mwa Gaza.
Mashambulizi ya mabomu mfululizo katika ukanda wa Gaza, yameingia siku ya sita leo tarehe 15 Mei 2021.
Licha ya mashambulizi hayo kuelekezwa kwa raia, Jeshi la Israel limekuwa likitoa taarifa kwamba linalenga kambi za waasi (Hamas).
Katika saa 24 zilizopita, ripoti zinasema jeshi la Israel limeua watu wazima 10 na watoto wanane.
Leo Jumamosi asubuhi, taarifa zinaeleza Wapalestina wanaendelea ‘kuokota’ miili ya watu walioangukiwa na jengo baada ya mashambulizi ya Israel.
Hata hivyo, chama tawala cha Hamas kimejibu mapigo kwa kuelekeza mashambuli ya maguruneti katika miji ya Askhelon na Ashdod, Israel.
Taarifa kutoka Israel zinasema, watu wanane wamefariki dunia kutokana na mashambulizi ya maguruneti kutoka Palestina.
Jeshi hilo limeeleza, mamia ya maguruneti yamekuwa yakirushwa kutoka Gaza yamekuwa yakielekezwa katika maeneo mbalimbali ya Israel.
Jumla ya Wapalestina 950 wameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika vurugu zinazoendelea mpaka sasa.
More Stories
Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu
NMB yafadhili wiki ya unywaji maziwa Katavi
#LIVE: Tuzo za EJAT2021, Majaliwa atoa ujumbe kwa MCT