ROEL Degamo (56), Gavana wa jimbo la katikati mwa Ufilipino pamoja na watu wengine watano, wameuawa jana Jumamosi, tarahe 4 Machi, kwa kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).
Hili ni shambulio la hivi punde dhidi ya maafisa wa serikali. Degamo, alikuwa gavana wa jimbo la Negros Oriental.
Polisi wamesema washukiwa sita waliokuwa wamebeba bunduki na waliovalia sare zinazofanana na zile zinazovaliwa na wanajeshi, waliingia katika nyumba ya gavana huyo aliyekuwa akitoa msaada kwa wananchi katika mji wa Pamplona na kuanza kufyatua risasi.
Rais wa Ufilipino, Ferdinand Marcos amelaani kile alichokitaja kuwa ni “mauaji” ya mshirika wake wa kisiasa.
Ameahidi kuwafikisha wahusika wa uhalifu huo mbele ya vyombo vya sheria.
Takriban wanasiasa watatu wameuawa kwa risasi tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Leave a comment