PAMBANO la mchezo wa ngumi lililofahamika kwa jina la ‘Payback Night’ kati ya mabondia, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ na Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’ limeahilishwa mara baada ya kukosekana kwa zawadi ya gari. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Pambano hilo awali lilipangwa kufanyika mwezi Julai, sasa litasogezwa mbele hadi tarehe 20 Agosti, 2021, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kucheza pambano hilo, tarehe 26 Mei, 2021.
Akizungumza na MwanaHALISI Online, promota wa pambano hilo, Suleman Semunyu amesema pambano hilo hii leo tarehe 13 Juni 2021, huku akieleza kuwa kushindwa kupatikana kwa zawadi ya gari kwa sasa ndio kumepelekea tukio hilo kutofanyika kwenye tarehe hiyo.
Alisema kuwa “Ni kweli pambano limehailishwa, unakumbuka licha ya kuwalipa fedha kama sehemu ya mshahara kwenye pambano hilo, nikatoa nyongeza ili wapate gari kama zawadi kwa mshindi wa pambano hilo.
Aidha Semunyu aliongezea kuwa zawadi hiyo imepeleka mbele mpambano huo, kwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na mtu ambaye alionesha nia ya kutoa gari hilo, lakini kwa muda uliobakia mpaka kufikia tarehe ya pambano hilo, haitawezekana.
“Nimeongea na mtu ambaye anaweza kuwa na nia ya kutoa gari, lakini kwa tarehe hiyo haitawezekana, bado tupo kwenye mazungumzo,” alisema promota huyo.
Promota huyo alisisitiza tarehe hiyo, mshindi kupata zawadi ya gari haitowezekana kama aliyeahidi wakati wa kuingia makubaliano hayo, lakini kama zawadi hiyo ikishindikana, pambano hilo litapigwa kwa kuwa haikuwa sehemu ya mapatano.
Pambano hilo litakuwa la pili kwa mabondia hao wenye uzito wa kati ‘Super Middle weight’ kufanyika ndani ya mwaka mmoja
Leave a comment