January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gari la Wengert labeba bangi

Gari la kampuni ya uwindaji ya Wengert Windrose Safaris (WWS) likiwa kituo cha polisi jijini Arusha huku likiwa limebeba magunia ya bangi

Spread the love

GARI la kampuni ya uwindaji ya Wengert Windrose Safaris (WWS) inayomilikiwa na wawekezaji wa Marekani, limekutwa na bangi na dereva wake anashikiliwa kwa uchunguzi. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).

Dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo ambaye ametambuliwa kwa jina la Frank Faustine, anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na bangi ipatayo magunia 11 iliyokamatwa majira ya saa 5 usiku juzi Jumanne, eneo la Ranchi, mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye barabara kuu ya Arusha-Namanga.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas ambaye alisema jana dereva huyo atafikishwa mahakamani na uchunguzi kuendelea kwa taarifa alizozitoa mpaka sasa.

Hakutoa maelezo zaidi lakini taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi leo asubuhi, zinasema dereva huyo ametaja baadhi ya viongozi wa kampuni ya WWS kuwa ndio wenye mali hiyo na kwamba aliagizwa kupeleka kwa “watu fulani” upande wa Kenya.

MwanaHALISI Online lilitaka kujua kwa ufasaha taarifa hizo lakini Kamanda Sabas alipotafutwa baadaye hakupatikana kwani simu yake iliita kwa muda mrefu bila ya kujibiwa.

Jana, baada ya taarifa za tukio hilo kuenea jijini Arusha, Aurelia Mtui, aliyejitambulisha kama Meneja Maendeleo ya Jamii wa WWS, alitoa taarifa kwa umma akisema kampuni hiyo imesikitishwa na tukio hilo.

Dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo ambaye ametambuliwa kwa jina la Frank Faustine
Dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo ambaye ametambuliwa kwa jina la Frank Faustine

Aurelia alisema dereva huyo amefanya kosa la utovu wa maadili na kinyume na sheria za nchi na kwamba wala halina uhusiano na kampuni.

Kampuni ya WWS ndiyo inayotajwa kama ya marafiki wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye Julai mwaka jana alisimamisha leseni za kumiliki kitalu hicho za Green Mile Safari (GMS) kwa madai ya kuvunja Sheria ya Wanyamapori.

Mpaka sasa, Waziri Nyalandu anashikilia mezani kwake rufaa ya GMS ya kupinga uamuzi wake wa kusimamisha leseni, iliyopelekwa Agosti 2014, huku akiwa tayari ameruhusu WWS watumie kitalu hicho bila ya kukitangaza ili wanaotaka waombe rasmi kama sheria inavyotaka.

WWS kupitia wafanyakazi wake ilivuruga shughuli za GMS ikiwemo ndege iliyobeba mizigo ya wageni kutoka Uarabuni, na kuvamia kambi katika kitalu hicho kitendo kilichosababisha wageni wahame.

error: Content is protected !!