Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Gambia wapiga kura kwa kutumia gololi
Kimataifa

Gambia wapiga kura kwa kutumia gololi

Spread the love

 

DUNIANI kuna mambo ya kushangaza, ndivyo unaweza kutafisiri Uchaguzi Mkuu wa Gambia baada ya kushuhudiwa wananchi wa taifa hilo lililo magharibi mwa Bara la Afrika wakipiga kura kwa kutumia gololi.

Licha ya kwamba katika chaguzi za karibuni kumeshamiri demokrasia nchini humo bado mfumo wake huo wa ajabu wa uchaguzi haujabadilika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana tarehe 4 Disemba 2021, wananchi wengi wa Gambia wamejivunia mfumo wao wa kipekee wa kupiga kura.

Ni kwamba katika upigaji kura huo wa kumchagua rais, karatasi za kupigia kura hazitatumika.

Badala yake, mpiga kura akifika katika kituo cha kupigia kura na baada ya kitambulisho chake kuthibitishwa, mpiga kura ataelekezwa kwenye safu ya ngoma zilizopakwa rangi za vyama vya wagombea tofauti.

Kinachochomoza kutoka juu ya kila ngoma ni bomba ambalo mpiga kura atapenyeza gololi aliyokabidhiwa na afisa wa uchaguzi.

Inatoa mlio wa kengele ili viongozi waweze kusikia kama kuna mtu yeyote atajaribu kupiga kura zaidi ya mara moja.

Wakati shughuli ya kupiga kura inapokamilishwa, gololi kutoka kwa kila pipa zinahesabiwa na kujumuishwa – kama inavyofanywa karatasi za kupiga kura.

Njia hii ya upigaji kura ilianzishwa baada ya uhuru mwaka 1965 kwa sababu ya kiwango cha juu cha watu wasiojua kusoma na kuandika nchini Gambia.

Marekebisho kadhaa yamefanywa tangu Rais wa zamani wa taifa hilo, Yayha Jammeh kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais mwaka 2016.

Jammeh aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1994, na kumuondoa madarakani kiongozi wa uhuru Dawda Jawara.

Waangalizi wengi wanaafiki kuwa uchaguzi pekee ambao Jammeh alishinda kwa haki ulikuwa wa mwaka wa 1996, wakati bado kulikuwa na kipindi cha fungate baada ya mapinduzi na kabla ya kuanza uongozi wake wa kimabavu.

Chaguzi zilizofuata zilichakachuliwa kwa maslahi yake, na kushindwa kwake 2016 kulionekana kumshangaza yeye na mrithi wake Adama Barrow.

Kwa kiasi kikubwa kinyang’anyiro kilikuwa mbio za farasi wawili, huku Barrow akiwa mgombea wa maridhiano aliyechaguliwa na muungano wa vyama vya upinzani. Mgombea wa tatu, Mama Kandeh, alipata asilimia 17 ya kura.

Rais Barrow anagombea tena, awamu hii kwa tiketi ya chama chake kipya.

Wagombea sita katika kinyang’anyiro hicho:

Rais aliye madarakani, Adama Barrow kutoka chama cha National People’s Party; Wakili ambaye alihudumu kwa muda mfupi kama makamu wa rais wa Barrow, Ousainou Darboe (United Democratic Party) pia alikuwa sehemu ya muungano uliomwangusha Jammeh na anagombea kwa mara ya tano.

Wengine ni Essa Mbye Faal (Mgombea Huru) -wakili na wakili kiongozi wa zamani katika TRRC iliyohitimishwa hivi karibuni. Anagombea urais kwa mara ya kwanza; Mama Kandeh (Gambia Democratic Congress) – Alikuwa wa tatu katika uchaguzi wa 2016, anaungwa mkono na Jammeh.

Wengine ni Abdoulie Ebrima Jammeh (National Unity Party) – mwalimu wa zamani aliyewahi kuongoza mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo. Anagombea kwa mara ya kwanza wakati Halifa Sallah (People’s Democratic Organisation for Independence and Socialism) ni mbunge anayegombea kwa mara ya tano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

error: Content is protected !!