July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Gamba la Kasa lamnyima dhamana

Spread the love

MBARAKA Mtambo (50) amepandishwa kizimbani kwa kosa la kusafirisha nyara za serikali alizokamatwa nazo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere, Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Akisoma mashitaka hayo Hanorin Mushi, Wakili wa Serikali mbele ya Helen Liwa, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, mtuhumiwa tarehe 7 Mei mwaka huu alikamatwa katika uwanja uo akiwa na magamba mawili ya Kasa mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mshitakiwa amekiri kutenda kosa hilo ambapo Hakimu Liwa alimwambia kuwa hatopata dhamana kutoka na kesi hiyo na kwamba, uamuzi utatolewa tarehe 19 Mei mwaka huu.

 

error: Content is protected !!