October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Gama ajikosha “udalali wa ardhi”

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amesema kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani kuwa anashiriki kupora ardhi ni uzushi na uongo mtupu. Anaandika Jimmy Mfuru … endelea.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio leo asubuhi, Gama amesema taratibu zote za kisheria zilifuatwa na kwamba wabunge wote mkoa wa Kilimanjaro walishirikishwa huku akidai kuwa ni sababu za kisiasa zinatumika kumchafua.

Akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi jana, Waziri Kivuli, Halima Mdee amesema kiongozi huyo kwa gharama za serikali aliwapelekawa wekezaji kwenya ardhi iliyolipiwa fidia kwa fedha za umma na kuanzisha kampuni binafsi ya Jun Yu Investments International Company Ltd.

Gama amesema yuko tayarikuchunguzwa kwa kuwa hana shaka kwani taratibu zilifanyika kisheria na wabunge wa mkoa huo walishiriki, hivyo anawashangaa kumgeuka.

error: Content is protected !!