January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gallawa: Jitokezeni kwa wingi kupiga kura

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa ametoa agizo kwa wananchi wote ambao wanasifa za kupiga kura wapige kura katika vituo ambavyo walijiandikishia. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Ghallawa alitoa kauli hiyo jana ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Amesema kutokana na maagizo ya Tume ya Uchaguzi kwa sasa watu wote wanatakiwa kupiga kura katika vituo vyao ambavyo wajiandikishia.

“Kama unajijua wewe ni mtanzania na unasifa za kupigakura piga kula ulipojiandikishia kama ulijiandikishia mkoani Mbeya na unaishi Dodoma tafadhari panda gari kapigie kura yako mkaoni Mbeya,” amesema Gallawa.

Aidha amewataka wananchi wenye sifa za kupigakura kuhakisha wanapigakura kwa amani na utulivu na kwa kuzingatia muda na kisha kurejea majumbani kwao baada ya kumaliza kupigakura.

Amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mablimbali waandae wanachama na wafuasi wao kwenda kupigakura bila kuvyonja sheria za uchaguzi, taratibu na kanunu zilizowekwa.

“Hairuhusiwi kwa mtu yoyote siku ya uchaguzi kufanya kampeni ya aina yoyote wala kuvaa mavazi ya chama chochote cha siasa,” amesema Gallawa.

Hata hivyo amesema maandalizi ya kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu kwa mkoa wa Dodoma yameshakamilika wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya zote saba wameshapokea vifaa vyote vitakavyotukika kwenye zoezi la uchaguzi.

Amesema mkoa wa Dodoma umefanikisha kuandikisha jumla ya wananchi 1,053,136, sawa na asilimia 102.74 ambapo amesema lengo lilikuwa kuandikisha wapigakura 1,025,084.

error: Content is protected !!