December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gairo wamuunga mkono Rais Samia kwa kupanda miti

Spread the love

KATIKA kuunga mkono harakati za Rais Samia Suluhu Hassan kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uongozi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro umekuja na mipango kabambe kupitia kauli mbiu ya ‘Urithi wa Kijani Gairo’ Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yameelezwa jana tarehe 8 Machi, 2022 na Mhifadhi Misitu wilaya ya Gairo, Robert Mwangosi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mipango ya wilaya hiyo katika kuboresha mazingira.

Amesema Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo wamejidhatiti kupanda miti kwa kuanzisha klabu mbalimbali za wanafunzi.

“Mbali na kuwaunganisha wanafunzi kupanda miti, pia tumeweka miundombinu ya kufanya wanafunzi wapende mazingira na tumefanikisha kila mwanafunzi kupanda mti mmoja tangu alipojiunga shule na atausimamia hadi atakapohitimu elimu yake,” amesema Mwangosi.

 

Naye Mkuu wa wilaya ya Gairo, Jabiri Makame amesema kampeni ya urithi wa kijani Gairo, ni kampeni ambayo inalenga kuibadilisha wilaya hiyo na kuwa ya kijani kwa kufanya harakati za upandaji wa miti.

Pia ni kampeni inayolenga kutoa elimu kwa jamii juu ya suala zima la uhifadhi wa mazingira ili wilaya hiyo.

error: Content is protected !!