Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Fundo rufaa ya Mbowe, Matiko kufunguliwa
Habari za Siasa

Fundo rufaa ya Mbowe, Matiko kufunguliwa

Freeman Mbowe na Ester Matiko wakipelekwa gerezani
Spread the love

HATMA ya rufaa ya Freeman Mbowe, Mwenyekti wa Chadema Taifa na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini itajulikana kesho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 28 Februari 2019 imeelezwa kuwa, hukumu ya rufaa ya serikali dhidi ya Mbowe na Matiko iliyokatwa na serikali inatarajiwa kutolewa kesho na Mahakama ya Rufaa.

Kesi ya msingi ilitajwa mbele ya Kelvin Mhina, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo.

Wakili Mwandamizi wa serikali, Simon Wankyo ameieleza mahakama kuwa, kesi hiyo imekuja kutajwa mpaka pale usikilizwaji wa rufaa kwenye mahakama ya rufani na mahakama kuu utakapohitimishwa.

Profesa Abdallah Safari, wakili wa utetezi amedai kuwa, shauri hilo limekuwa likifika kwa ajili ya kutajwa na kisha kuahirishwa kwa sababu ya rufaa zilizokatwa na serikali yenywe.

“Nashangaa kila siku shauri linaahirishwa kwa sababu ya rufaa walizokata wenyewe ambapo hawaielezi mahakama mwenendo wa rufaa zao.

“…sisi tumepewa taarifa kuwa, kesho saa tatu asubuhi Mahakama ya Rufaani itatoa hukumu ya rufaa yao lakini hawaipi mahakama taarifa,”amedai Prof. Safari.

Wankyo ameieleza mahakama kuwa, yeye hana taarifa hiyo ambapo Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 14 Machi mwaka huu.

Rufaa hiyo iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) imelenga kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa tarehe 30 Novemba mwaka jana, kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana.

Shauri hilo linasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Gerald Ndika, Stella Mgasha na Mwanaisha Kwaliko uliwsilisha hoja mbili za kuomba rufaa namba 344 ya Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika iondolewe mahakani.

Hoja za upande wa serikali juu ya rufaa hiyo ni kwamba, mahakama kuu haikuwapa muda wa kusikilizwa wakati usikilizwa wa rufaa ya kina Mbowe.

Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu akisaidiwa na Paul Kadushi aliwasilisha hoja hizo ambapo ameiomba mahakama kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa, haina miguu ya kisheria na kwamba, ni kinyeme cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Nchimbi alidai kuwa, Jaji Rumanyika alipotoka kisheria kwa kuipanga na kuiita kwa ajili ya usikilizwaji huku akijua rufaa hiyo iliwasilishwa kinyume na kifungu cha 362 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo 2002.

Alidai kuwa, Jaji Rumanyika hakuwapatia muda na haki ya kutosha wa kuuzikiliza upande wao.

Peter Kibatala, wakili wa upande wa utetezi alijibu hoja za mawakili wa serikali alidai, Mahakama Kuu haikusikiliza rufaa iliyokuwepo mahakamani zaidi ya kusikiliza pingamizi ziliyowasilishwa na upande huo.

Kibatala alidai kuwa, rufaa hiyo haina mashiko na kuiomba mahakama hiyo kuitupilia mbali.

Mbowe na Mtiko walifutiwa dhama yao tarehe 23 Novemba mwaka jana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kueleza kuwa, walikwenda kinyume na masharti ya dhamana kwenye kesi ya  msingi ya uchochezi inayowakibili.

Katika kesi ya msingi, Mbowe Matiko na wengine saba wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

Wengine ni Mbunge wa Peter Msigwa, Iringa mjini; John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji.

Pia wamo Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!