Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Fukuto lapanda uchaguzi TLS
Tangulizi

Fukuto lapanda uchaguzi TLS

Dk. Edward Hoseah, mgombea Urais TLS
Spread the love

 

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa Kanda na Umoja wa Vijana Wanasheria. Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

Chaguzi hizo zitafanyika leo Jumatano tarehe 14 Aprili 2021, kuanzia saa nane mchana hadi 10 alasiri, katika Ukumbi wa Lush Garden, jijini Arusha.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Kaleb Lameck Gamaya amesema, chaguzi hizo zitatanguliwa na uchaguzi wa vijana.

“Kuna shughuli ya kuchagua viongozi. Kila mwaka TLS kinabadili uongozi sababu chama ni wanachama na kila mwanachama ana fursa ya kukitumikia chama.

Albert Msando, mgombea Urais TLS

“Wanafanya kazi kwa kujitolea kwa mujibu wa wito wa kisheria na taaluma, lazima utumikie chama. Utumishi wao si wa kulipwa mapesa mengi,” amesema Gamaya.

Kuhusu uchaguzi wa vijana, Gamaya amesema viongozi watakaochaguliwa ni mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa chama hicho.

“Leo tuna chaguzi mbili, uchaguzi wa mwenyekiti, makamu mwenyekiti wa vijana utaanza saa nane hadi tisa na nusu mchana,” amesema Gamaya.

Shehzada Walli mgombea Urais TLS

Amesema, watakao gombea nafasi hiyo ni vijana wasiozidi umri wa miaka 35,  ambao wamefanya kazi ya uwakili kuanzia miaka miwili na kuendelea.

Kwa upande wa uchaguzi wa kanda, Gamaya amesema viongozi watakaochaguliwa ni wa kanda saba za TLS.

Kanda hizo ni Mzizima, Bagamoyo, Kaskazini, Nyanda ya Juu, Ziwa, Kati na Magharibi.

Amesema, kuna kanda ambazo kuna mgombea mmoja, ambao watapigiwa kura ya ndio au hapana. Kanda hizo ni Bagamoyo na Kaskazini.

Gamaya amesema, viongozi watakaochaguliwa kwenye chaguzi hizo, wataapishwa Jumamosi tarehe 17 Aprili mwaka huu.

Uchaguzi wa rais wa chama hicho unatarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 17 Aprili 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!