Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Fredrick Sumaye aviponda viwanda vya Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Fredrick Sumaye aviponda viwanda vya Magufuli

Spread the love

WAZIRI Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano, Fredrick Sumaye amesema, nchi kwa sasa inaendeshwa “kiholela,” na kudai kuwa ikiwa chama chake kitafanikiwa kushika madaraka, kitaimarisha uchumi. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Amedai kuwa kwa sasa, uchumi wa taifa unaporomoka na kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli, “imeamua kwa makusudi kuvuruga uchumi.”

“…huwezi kuzungumzia viwanda wakati uchumi umelemaa. Ndio maana hivi sasa, mtu anamiliki vyerahani vinne, lakini anaambiwa anamili kiwanda,” ameeleza.

Amesema, “tunajidanganya. Hatuwezi kuzungumzia viwanda bila kuwapo uchumi; na kwamba uchumi wenyewe ndio viwanda.”

Sumaye ametoa kauli hiyo leo Jumanne jijini Dar es Saalaam, wakati wa uzinduzi wa “sera mpya” za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Amesema, kila anayetaka urais, sharti aeleze wananchi sera zake na ataifanyia nini nchi hii. Chadema kinazindua sera hizo ambazo zitapelekwa kwa wananchi na kunadiwa.

Sumaye amekuwa waziri mkuu kwa muda wa miaka kumi mfululizo katika kipindi cha utawala wa Benjamin Mkapa.

Katika kipindi cha uongozi wake, uchumi wa nchi ambao ulikuwa hoi kutokana na kutengwa na mashirika ya kimataifa – Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) , uliimarika kwa kasi.

Aidha, ni katika kipindi hicho, mfumuko wa bei ulipungua, ajira zilipatikana, elimu imeboreshwa na hospitali zote zilikarabatiwa na kuwa na dawa.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali, akiwamo mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini, Chadema kimesema, kimeamua kuchukua hatua hiyo ili kujitofautisha na chama kilichopo madarakani.

Naye Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho taifa amesema, sera ya Chadema ya sasa imezingatia namna ya uboreshaji wa uchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!