Klabu ya soka ya Frankfurt ya nchini Ujerumani imefanikiwa kutwaa ubigwa wa Europa League msimu huu wa 2021/2022 baada ya jana kuifunga Rangers ya katika Fainali ya michuano hiyo. Anaripoti Damas Ndelema Tudarco ( endelea).
Fainali hiyo ilioisha kwa sare ya bao moja kwa moja kabla ya kwenda kwenye mda wa nyongeza na hatimae mikwaju ya penalti na Frankfurt kufanikiwa kuibuka na ushinda baada ya kufanga penalti tano na Rangers kukosa penalti moja aliyokosa kiungo wa zamani wa vilabu vya Arsenal na Juventus Aron Ramsey
Frankfurt walifika hatua hiyo ya Fainali baada ya kuitoa Barcelona na Westham katika hatua ya robo fainali na nusu fainali huku kwa upande wa Rangers walifika hatua hiyo kwa kuitoa Braga na Rb Leipzing
Fainali hiyo inakua fainali ya pili mfululizo kufika hadi kwenye changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya fainali ya msimu uliopita kati ya Manchester United na Villareal kwenda hadi hatua ya penalti na Villareal kuibuka bigwa wa michuano hiyo
Leave a comment