January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Fomu za Urais Chadema Sh. 1 mil

Kamati Kuu ya Chadema

Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza gharama za fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwa ngazi ya Udiwani, Uwakilishi, Ubunge na Urais. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi habari, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim amesema fomu za wagombea wanaowania nafasi ya Urais zitatolewa kwa Sh. 1,000,000, Ubunge wa Jimbo na Viti Maalum Sh. 250,000, Udiwani wa Kata na Viti maalum Sh. 50,000.

Mwalim amesema, fomu hizo zitaanza kutolewa kuanzia Mei 18, 2015, ambapo mtia nia wa nafasi ya Urais ataweza kuchukua eneo lolote katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya na Jimbo. Ila kwa upande wa Wabunge na Madiwani wataweza kuchukua fomu kwenye ngazi ya jimbo, wilaya na kata.

“Fomu hizo pia zitapatikana mitandaoni kupitia website ya Chama, tumefanya hivyo ili kuondoa usumbufu kwa wanachama ambao hawako katika mikoa yao labda mtu amesafiri kikazi awaze kupata,” amesema Mwalim.

Hata hivyo Mwalim amesema, fomu ni lazima zirejeshwe kwenye jimbo au kata ambayo Mgombea anagombea na ndipo atapaswa kulipa gharama za fomu husika.

Mwalim amesema, kwa upande wa Wabunge wa viti maalum, zitalipiwa moja kwa moja kwenye akaunti ya BAWACHA Taifa ambayo ipo kwenye fomu husika, hivyo wagombea wa nafasi hizo watalazimika kuambatanisha fomu zao na risiti ya Benki ikionesha imelipwa.

error: Content is protected !!