July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Fluoride yaathiri maji mikoa sita

Naibu wa Waziri wa Maji, Amos Makala akijibu hoja bungeni

Spread the love

MIKOA ya Kilimanjaro, Manyara, Singida, Mwanza na Arusha, imetajwa kuwa kati ya mikoa ambayo ina vyanzo vya maji vingi vyenye madini mengi ya fluoride. Anaandika Dany Tibason … (endelea)

Hayo yamebainishwa bungeni na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Rebeca Mngodo (Chadema).

Mbunge huyo alitaka serikali ieleze ina juhudi gani kwa ajili ya kuwanusuru wananchi wa Wilaya ya Meru, kata ya maji ya Chai kutokana na kutumia maji ambayo yana kiasi kikubwa cha madini hayo.

“Baadhi ya wananchi waishio katika Wilaya ya Meru, kata ya maji ya Chai na maeneo ya Ngurudoto wanapata athari mbaya ya afya ya kuwa na meno ya rangi na miguu ya matege kutokana na maji kuwa na madini ya fluoride iliyozidi.

“Na niwajibu wa serikali kuhakikisha watu wake wanapata maji safi na salama kutokana na kodi wanazolipa. Je, serikali imefanya nini kukabiliana na tatizo hilo,”amehoji Mngodo.

Akijibu swali hilo, Makala amesema kuwa mikoa 6 nchini inakabiliwa na wingi wa madini hayo katika maji jambo ambalo serikali imejaribu kutafuta ufumbuzi wa kutafuta vyanzo vingine vya maji salama tofauti na hayo.

Mbali na hilo, amesema katika wilaya ya Meru, vyanzo 121 vimebainishwa na kuhakikiwa ubora wake na matokeo yameonesha kuwa asilimia 55 ya vyanzo hivyo vina kiwango cha madini hayo chini ya asilimia miligramu nne kwa lita moja, inayokubalika kimataifa.

Amesema kuwa, serikali inaendelea kupambana na tatizo hilo ili kuhakikisha Watanzania wanapata maji safi na salama ili kupunguza matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwa watumiaji.

error: Content is protected !!