February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Filamu ya Ndugai na wabunge yaendelea Dodoma

Job Ndugai,. Spika wa Bunge la Tanzania

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema  mbunge wa Ubungo Saed  Kubenea hajaitwa kwenye Kamati Ulinzi na Usalama ya Bunge kama mtuhumiwa wa kitu chochote, anaandika Hamis Mguta.

Ndugai amesema hayo leo bungeni akieleza kauli iliyotolewa na Mbunge wa  Arusha Mjini,  Godbless Lema akimshtumu Spika kuhusu sababu za kuwaita mbunge Kubenea na Zittp Kabwe kwenye kamati hiyo.

Amesema Bunge liliamua kuwa maombi yanayohusiana na usalama yaende kwenye kamati ya ulinzi baada ya Mbunge wa Nzega mjini, Husein Bashe (CCM),  kutoa ushauri huo.

“Hayo aliyoyasema Kubenea yanaweza kuisaidia kamati katika kazi zake, kwa hiyo kupelekwa Kubenea kwenye kamati ile hapelekwi kama mtuhumiwa wa kitu chochote.

“Anapelekwa ili anayoyasema barabarani ayaseme hapa kama mbunge,” amesema Ndugai.

Pamoja na kumshutumu Spika huyo,  akiwa mjini  Nairobi Lema alitaka Bunge kusimama baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu kupigwa risasi akiwa Dodoma.

Ndugai amesema kuwa maombi hayo ya Lema kutaka Bunge lisimame baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi si vizuri kwa kuwa hakuna kanuni zinazotaka hivyo isipokuwa  zinasema Mbunge akifariki ndiyo  litasimama kwa siku moja.

Awali Ndugai aliagiza Kubenea ajisalimishe popote alipo ili ahojiwa kwa madi ya kumuita Spika muongo.

Baada ya kutokea tukio baya la Lissu kupigwa risasi, Ndugai aliliambia Bunge idadi tofauti ya risasi alizopigwa huku  Kubea naye akitoa idadi nyingine isiyonana na ya kwake  kitendo ambacho Spika aliona kama mbunge huyo aliomuona yeye ni muongo.

error: Content is protected !!