Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Michezo Messi amponza Rais wa Soka Palestina, afungiwa miaka 12
Michezo

Messi amponza Rais wa Soka Palestina, afungiwa miaka 12

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), kupitia kamati yake ya nidhamu imemfungia miaka 12, Rais wa Chama cha Soka cha Palestina, Jibfril Rajoub kutojihusisha na mchezo wa soka pamoja na faini kiasi cha Euro 15,826 baada ya kuagiza kuchomwa moto kwa jezi ya Messi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Adhabu hiyo imekuja baada baada ya rais wa chama soka cha Parestina kuaandikia barau Shirikisho la Soka Argentina akiwataka wasimchezeshe Lionel Messi katika mchezo wa kirafiki kati ya Argentina na Israel uliopangwa kuchezwa katika mji wa Jerusalem.

Na kama watakiuka tamko lake na Messi kuonekana mjini Jerusalem katika mchezo huo basi mashabiki wa soka nchini Palestina watafute jezi za nyota huyo popote pale nchini Palestina na wazichome moto.

Hata hivyo mchezo huo kati ya Argentina na Israel haukufanikiwa kucheza kutokana na kuhofia usalama wa wachezaji wao, kutokana na jambo hilo kuonekana kisiasa zaidi kutokana na nchi hizo mbili kuwa katika mvutano kwa miaka mingi sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!