Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo FIFA yamfungia maisha kiongozi CAF
Michezo

FIFA yamfungia maisha kiongozi CAF

Kwesi Nyantakyi
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpiwa wa Miguu Duniani (FIFA) limemfungia maisha kujihusisha na masuala ya soka aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini Ghana (GFA), Kwesi Nyantakyi baada ya kukutwa na hatia ya kupokea rushwa ya kiasi cha dola 65,000 kutoka kwa mwandishi wa shirika la habari la England, Anas Aremeyaw. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endeleaa). 

Shirikisho hilo lilifanya uchunguzi kwa kina kujua kama kweli alihusika kupokea kiasi hicho cha pesa kutoka kwa mwandishi huyo ambaye alitumwa kwa kazi maalum ya kupima uaminifu wa rais huyo na baadaye kumkuta na hatia na kuchukua maamuzi hayo.

Baada ya tuhuma hizo Nyantakyi ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na mjumbe wa halmashauli kuu ya Fifa alijiuzuru nafasi yake ya urais GFA mwezi juni na kujivua nyadhifa zake zote za CAF na FIFA ingawa hakuna mahari alipo kubali kuwa alipokea kiasi hicho cha fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!