August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

FIFA yaipongeza Serengeti Girls

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA), limeipongeza Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa kufanikiwa kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia kwa wasichana chini ya Umri wa miaka 17. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Tanzania imefuzu kwenye fainali hizo kupitia timu ya Taifa ya wasichana Serengeti Girls, mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Cameroon uliofanyika jumapili tarehe 5 Juni 2022.

Kabla ya mchezo huo, kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Cameroon Serengeti Girls ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, wakiwa ugenini.

Shirikisho hilo limeipongeza TFF, kupitia barua yao iliytumwa na mkurugenzi wa mashindano Manolo Zubiria kwenda kwa mtendaji mkuu wa TFF, Wilfred Kidao.

Fainali hizo zitafanyika Oktoba mwaka huu, nchini India kwenye miji ya Navi Mumbai, Goa na Bhubaneswar ambapo kwa nchi za Afrika, Serengeti Girls itaungana nan chi za Morocco pamoja na Nigeria.

error: Content is protected !!