
Asante Kwasi (kushoto) alipokuwa Simba
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeifungia klabu ya Simba kusajili katika kipindi kimoja cha dirisha hilo kufuatia kutiwa hatiani kwa kutomlipa stahiki zake aliyekuwa beki wao raia wa Ghana, Asante Kwasi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Adhabu hiyo imekuja kufuatia FIFA kujiridhisha kuwa Simba haikufanikiwa kumalizana na beki huyo baada ya kuachana naye mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2018/19 na kutakiwa kumlipa mchezaji huyo kiasi cha Sh. 25 milioni.
Simba itaanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia msimu ujao katika dirisha kubwa la usajili litakalofunguliwa mara baada ya Ligi kumalizika.
Kwasi alijiunga na Simba mwaka 2017 akitokea klabu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
More Stories
Mourinho aingia kwenye rekodi mpya barani Ulaya
Mayele atetema Mwanza, mabao 14 sawa na Mpole
Kim aita 28 Stars