SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Dunia (Fifa) kupitia wajumbe wake, wamefikia makubaliano ya kuongeza idadi za timu kufikia 48 kutoka 32 zilizokuwa zikishiriki Kombe la Dunia hapo awali, na utaratibu huo utaanza kutumika katika fainali za mwaka 2026.
Fifa wamefikia hatua hiyo baada ya kupiga kura katika mkutano mkuu wa uliofanyika Zurich ambapo kwa sasa timu 48, zitakuwa katika makundi 16 na kila kundi litakuwa na timu tatu na sio nne kama ilivyokuwa hapo awali.
Timu mbili za juu zitafuzu katika hatua ya 32 bora na idadi ya mechi zitaongezeka kufikia 80 badala ya 64 na michuano hiyo itachezwa kwa siku 32.
Lengo la kuongeza idadi ya timu katika michuani hiyo ni kufanya mchezo wa mpira kuendelea duniani kote na kuongeza washiriki kutoka mabara ambayo yalikuwa na idadi ndogo ya timu katika kombe hilo.
Hii ni mara ya pili kwa FIFA kuongeza idadi ya timu shiriki katika michuano hiyo baada ya mwaka 1998, katika fainali zilizofanyika Ufaransa ushiriki wa timu uliongezeka kutoka 24 mpaka 32 ambazo zitafikia kikomo 2022 katika fainali zitakazofanyika Quatar kabla ya kuanza kwa utaratibu mpya 2026.
Leave a comment