November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

FIFA waomba vita kati ya Russia, Ukraine isitishwe kupisha Kombe la Dunia

Gianni Infantino

Spread the love

 

RAIS wa shirikisho la kandanda duniani, Gianni Infantino ametoa wito wa kusitishwa kwa muda wa mwezi mmoja vita kati ya Urusi na Ukraine ili kupisha mashindano ya kombe la dunia yanayofanyika nchini Qatar. Inaripoti Mitandao ya Kijamii … (endelea).

Kiongozi huyo wa FIFA alisema hayo jana tarehe 15 Novemba, 2022 wakati wa chakula cha mchana kwenye mkutano wa viongozi wa mataifa 20 tajiri duniani G20 mjini Bali Indonesia.

Akiwahutubia viongozi hao, Infantino amesema kwamba mashindano ya kwanza ya kandanda duniani kufanyika mashariki ya kati yanaweza kuchochea kuchukuliwa hatua chanya, ili kuwasilisha ujumbe wa matumani.

Urusi ndio iliandaa michuano ya mwisho ya kombe la dunia 2018 na ikafika robo fainali, wakati Ukraine ni miongoni mwa nchi zinazojaribu kuanda fainali za mwaka 2030.

error: Content is protected !!