September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Fidel Castro: Nakaribia mwisho 

Spread the love
FIDEL Castro, kiongozi mwanzilishi na mwanamapinduzi wa chama tawala cha   kikomunisti nchini Cuba, amesema kuwa anakaribia mwisho wa maisha yake, anaandika Wolfram Mwalongo.
Amesema, wananchi na viongozi wa taifa hilo wanapaswa kuyatumia mawazo yake katika kuendesha nchi hiyo.
Castrol amesema maneno hayo leo wakati akihutubia wananchi wa tarifa hilo akiwa anatimiza miaka 90.
“Nakaribia mwisho wa maisha yangu, nimekipa nguvu chama hiki kwa nusu karne hivyo  mawazo yangu myatumie kama ushahidi na kubaki katika mapinduzi,” amesema Castro.
Raul Castro (84), mdogo wa Fidel amesmthibitishia kiongozi huyo kuwa,  anatarajia kuongoza tena muhula mwingine wa miaka mitano na kwamba, wataendelea kuenzi mapinduzi hayo.
error: Content is protected !!