January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

FFU wawashushia kipigo Wabunge wa Ukawa

Spread the love

ASKARI polisi zaidi ya 40 wamevamia ukumbi wa bunge huku baadhi yao wakitembeza kichapo na kutoa maneno machafu kwa wabunge wa Ukawa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo ilijitokeza baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kujibu hoja ya mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) ambaye alitaka kujua ni kwanini serikali inasitisha kurushwa matangazo ya moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Akijibu hoja Chenge amesema kamati ya uongozi imekubaliana suala hilo lisiendelee kujadiliwa na badala yake mjadala wa kujadili hotuba ya rais uendelee.

Hali hiyo ilizua kizaazaa ambapo mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Mbunge wa Msoma Vijijini, John Heche (Chadema) kuomba mwongozo ambao haukupata majibu.

Kutokana na hali hiyo kwa zaidi ya mara tano wabunge wa Ukawa waliendelea kusimama jambo ambalo lilimfanya mwenyekiti kuwataja wabunge, Lissu, Ester Bulaya, Heche, na Godbless Lema waondolewe bungeni na askari wa Bunge.

Vurugu ziliibuka baada ya Lema kugoma kuondoka ukumbini wala kuondolewa na badala yake ataondoka ukumbini akiwa maiti kwani yeye alikuwa hajaomba mwongozo wala kufanya fujo.

Kutokana na kauli hiyo wabunge wote wa Ukawa walilazimika kusimama huku jeshi la polisi waliovaa sale 32 huku wale askari waliovaa kiraia wakiwa zaidi ya 20.

Jambo hilo lilimfanya mwenyekiti kusimamisha bunge kwa dakika 10 na muda mfupi waliongezeka askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU.

Hali iliendelea kuwa tete huku askari polisi wakitumia lugha chafu kwa wabunge wanawake ambapo hata wabunge hao walirushiana maneno na askari hao.

Katika sekeseke hilo lilisababisha mbunge mmoja wa Ukawa, Zubeir Kuchauka wa Jimbo la Liwale ambaye alizolewa mzobe mzobe na askari na kuvuliwa koti, shati na viatu na kubaki na fulana, suruali na soksi.

Naye Sabrina Sungura alikumbwa na adha hiyo kwa kuibiwa kikuku mkufu na kuvuliwa mavazi yake ya yanayomtambulisha kwa imani yake ya kiislam na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari.

Kizaazaa hicho hakiwakumba wabunge pekee wa Ukawa pekee, pia kilifika mpaka kwa waandishi wote waliamlishwa kuondoka katika vyumba vyao vya habari huku wakizuiliwa kupiga picha na wale walioonekana kupiga kura walilazimishwa kuzifuta.

Kama hiyo haitoshi waandishi walifungiwa milango ili wasikutane na mbunge yeyote aliyetolewa nje.

Nje ya ukumbi wa bunge zaidi ya magari mawili yenye FFU yakiwa na askari ndani yake yalikuwa yametanda.

error: Content is protected !!