March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Fellaini ashika namba nne kulipwa mshahara mnono Man United

Spread the love

KIUNGO wa Manchester United ambaye ni raia wa Ubelgiji, Marouane Fellaini, ameongezewa mshahara unaomfanya ashike namba nne kati ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwa wiki kwenye klabu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni shabiki mkubwa wa kocha wa klabu yake, Jose Mourinho, amefanikiwa kushawishi mabosi wake na sasa kwa wiki atakuwa analipwa kitita cha Pauni za Uingereza 150,000 (sawa na Sh. 448 millioni) baada ya makato ya kodi.

Kwa mshahara huo, Marouane Fellaini anakuwa nyuma ya Alexis Sanchez, Paul Pogba na Romeu Lukaku.

error: Content is protected !!