Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Fedha za maendeleo yavuruga mkutano
Habari Mchanganyiko

Fedha za maendeleo yavuruga mkutano

Spread the love

MWENYEKITI wa kijiji cha Kikundi, kata ya Tomondo, Morogoro, Musa Muhongo ameahirisha mkutano mkuu wa kijiji mara baada ya wanakijiji kuchachamaa wakidai kuelezwa zilipo fedha za maendeleo. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Wananchi hao wanadau kujua zilipo Sh. 200,000 zilizobaki kati ya Sh. 1.2 milioni walizotoa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha kata ili kusaidia jamii ikiwemo mama na mtoto.

Mwenyekiti huyo alifikia hatua hiyo jana mara baada ya wananchi hao zaidi ya 500 kukataa kuendelea kwa mkutano huo ambao ndio kwanza ulikuwa katika hatua ya kusomwa yatokanayo wakidai Mtendaji wa Kata, Jotham Sanga awape ufafanuzi kufuatia idadi ya matofali yaliyonunuliwa  kutolingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Mmoja wa wanakijiji hao Saidi Mpinzi alisema, walitakiwa kila kijiji kati ya vijiji vinne vilivyopo kwenye kata hiyo kutoka matofali 12,500 baada ya kupitisha michango nyumba kwa nyumba lakini wao waliamua kutoa akiba ya kijiji kiasi cha Sh. 1.2 milioni ambayo walielekeza kwenye ununuzi wa matofali hayo ambayo yamenunuliwa matofali 10,000 badala ya 12,500.

Aidha Mpinzi alisema, kufuatia sintofahamu ya idadi ya matofali na fedha waliamua kuhesabu matofali na kukuta idadi hiyo pungufu huku wakibaini ukosefu wa matofali ya vijiji vingine vitatu kama walivyokubaliana.

Akizungumzia hilo, Mtendaji kata wa kata hiyo Jotham Sanga alisema, wananchi hao wameshindwa kumuelewa kwani yeye aliweza kununua matofali hayo na ukweli wa fedha zilizobaki na makusanyo ya fedha za vijiji vingine yatapatikana mara baada ya kikao cha kamati ya maendeleo ya kata.

Sanga alisema wanakijiji hao hawana budi kuwa na subira wakati wakitaka maendeleo kwani suala la fedha, makusanyo na matumizi huwa na mipangilio yake ambayo hutolewa kwa awamu.

“Fedha zilizobaki kama zipo zitakuwepo kwenye kamati na vijiji vingine vimeshaanza kukusanya na tunanunua matofali kwa awamu kulingana na uwepo wa fedha ya usafirishaji,” alisema Sanga.

Naye Diwani wa Kata ya Tomondo, Hamisi Msangule aliwataka wanakijiji hao kuwa na subira hadi watakapopewa majibu wanayohitaji lakini aliwaasa kutoacha kuchangia shughuli za maendeleo.

Msangule alisema, kufuatia mafunzo waliyopata kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP- Mtandao) wameweza kuona umuhimu wa kuinua afua za kijinsia kwa kuanzia na ujenzi wa kituo cha afya ili kumsaidia mama na mtoto.

Alisema, kupitia baraza la maendeleo la kata vijiji vinne vya kata hiyo ambavyo ni Kikundi, Kungwe, Lukonde na Mvuleni vimekubaliana kujenga kituo cha afya katika eneo la Zahanati ya kijiji cha Kikundi kwa kutoa matofali 12,500 kwa kila kijiji na hivyo kufikia matofali 50,000 kwa kata nzima kwa ajili ya kuanza ujenzi wa wodi ya kinamama wajawazito, watoto na Leba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!