Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Fedha za COVID-19: IMF yaitega Tanzania
Kimataifa

Fedha za COVID-19: IMF yaitega Tanzania

Spread the love

 

SHIRIKA la Fedha Duniani (IMF), limesema liko tayari kuipatia mkopo wa dharura wa Dola za Marekani 574 milioni (Sh. 1.3 trilioni), Serikali ya Tanzania, endapo itatoa takwimu za hali ya ugonjwa wa homa kali, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini Tanzania, Jens Reinke, katika mahojiano yake na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), yaliyofanyika hivi karibuni.

Mkuu huyo wa IMF Tanzania, amesema mikopo hiyo ya dharura ya kukabiliana na COVID-19, hutolewa kwa nchi zinazokidhi vigezo vya shirika hilo, ikiwemo utoaji wa takwimu, ambazo zitawasilishwa katika bodi yake.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Serikali ya Tanzania, kuomba tena mkopo huo Machi 2021, baada ya ombi lake la kwanza kukataliwa na IMF, kufuatia nchi hiyo kutokidhi vigezo vya kupata mkopo huo.

Reinke amesema, IMF na Serikali ya Tanzania, inaendelea na majadiliano juu ya maombi hayo, kwa ajili kufikia muafaka wa utolewaji mkopo huo.

“Uwepo wa takwimu ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na janga hili. Zitawasilishwa kwenye Bodi ya IMF, kabla ya kuthibitishwa. Kwa hiyo, kuwa na takwimu za msingi, ni kigezo cha moja kwa moja . Hatuko karibu sana kuidhinisha chochote kwa Tanzania, tunaendelea na majadiliano,” amesema Reinke.

Tangu mlipuko wa virusi hivyo utokee Tanzania Machi 2020, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Hayati John Magufuli, ilitoa takwimu hizo kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo mara ya mwisho zilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mwishoni mwa Aprili mwaka huo.

Hata hivyo, baada ya Rais wa Awamu ya Sita wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, kuingia madarakani Machi 2021, aliunda kamati ya kuchunguza mwenendo wa ugonjwa huo, ambayo iliishauri Serikali yake itoe takwimu hizo.

Rais Samia aliingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, baada ya Magufuli kufariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Mwili wa Magufuli ulizikwa nyumbani kwao Chato, mkoani Geita, tarehe 26 Machi 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

error: Content is protected !!