August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Fedha za Bombadier zingejenga hospitali za Ocean Road tano

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier

Spread the love

MBUNGE wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema) amesema anasikitisha kuona serikali inakimbilia kutoa mabilioni ya fedha kununua ndege wakati hali ya afya ni mbaya nchini, anaandika Dany Tibason.

Mwakajoka alitoa kauli hiyo bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka wa fedha 2017/18.

Mbunge huyo akichangia amesema kwa sasa hali ya vituo vya afya vina hali mbaya kutokana na kukosekana na vifaa muhimu vya matibabu.

Amesema inasikitisha kuona hospitali nyingi za mikao hazina CT-Scan na MRI kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama na watoto kwa lengo la kuboresha afya za kada hiyo.

Amesema vipimo hivyo vimekuwa vikipatikana kwa gharama kubwa jambo ambalo linaonesha zaidi kuwa serikali inafanya biashara badala ya kutoa huduma inayostahili kwa jamii.

Amesema anashangazwa na serikali ikishindwa kutoa kipaumbele katika swala la afya na badala yake wameelekeza fedha nyingi katika ununuzi wa ndege ya Bombadia ambayo ingeweza kuwa na uwezo wa kujenga zahanati kila kanda zenye adhi ya hospitali ya Ocean Road.

Amesema kutokana na kutokuwa na zahanati pamoja na vituo vya afya vya uhakika watanzania wengi wanakufa kwa ugonjwa wa kansa ambapo taarifa zinaonesha kuwa ifikapo 2020 watu wengi watakufa kwa kansa zaidi.

Mwakajoka amesema umefika wakati sasa wa serikali kuona uwezekano wa kupunguza fedha katika maeneo ambayo hayana umuhimu na badala yake waelekeze fedha hizo katika sekta ya afya.

Aidha amesema hakuna njia yoyote ya kupunguza vifo vya akina mama na watoto kama hakuna zahanati za kutosha wala vituo vya kutosha vya afya.

Amesema kwa sasa kuna upungufu wa hospitali 20 nchi nzima vituo vya afya upungufu ni 3913 na zahanati kuna upungufu wa zahanati 8075.

error: Content is protected !!