Saturday , 3 June 2023
Home Kitengo Michezo FCC bado yaikalia kooni Simba
Michezo

FCC bado yaikalia kooni Simba

Mohammed Dewji 'MO'
Spread the love

TUME ya Taifa ya Ushindani (FCC) imetoa taarifa kwa umma juu ya kuendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ya Simba kutoka umiliki wa wanachama hadi kuendeshwa kama kampuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tume hiyo ambayo imeanzishwa chini ya kifungu namba 62 cha sheria ya ushindani namba nane ya mwaka 2003, inafanya uchunguzi juu ya muunganiko wa makampuni ambayo yanakwenda kubadilisha mfumo wa uendeshaji ndani ya klabu ya Simba bila kutoa taarifa kwenye tume hiyo.

Taarifa ambayo imetolewa na tume hiyo hii leo tarehe 15 Januari, 2021 kupitia gazeti la Serikali imezitaja kampuni hizo ni kuwa Simba Sports Club Holding Company Limited ambaye ni mdawa namba moja, MO Simba Company Limited kama mdawa namba mbili, Simba Sports Club Company, mdawa namba tatu, Simba Sports, mdawa namba nne na Mohammed Gulamabbas Dewji akiwa mdawa namba tano.

Katika tuhuma hizo FCC imegundua kuwa katika mchakato huo wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo kuwa mdawa namba namba tatu ambaye ni Simba Sport Club Company, akishirikiana na mdawa namba moja Simba Sports Club Holding company sambamba na mdawa wa pili MO Simba Company Limited, pamoja na mdawa wa tano Mohammed Dewji walichukua nembo ya kibiashara ambayo inamilikiwa na klabu ya Simba.

Kikao cha Bodi ya Simba

Kitendo hicho kiliashilia kubadilika kwa umiliki wa mali na biashara za klabu ya Simba bila kuitaarifu tume hiyo jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 11(2) kikisomwa pamoja na kifungu cha 11(6) cha sheria ya ushindani.

Mara baada ya FCC kuchunguza muunganiko wa makampuni hayo imetoa nafasi kwa yoyote kati ya kampuni hizo tano kufikisha malalamiko kwa maandishi kama ataona muunganiko huo utaweza kuathiri maslahi yake katika mchakato huo.

Kuibuka huku kwa FCC kumetokana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba Mohammed Dewji kueleza kuwa mchakato wa mabadiliko wa klabu hiyo umekwamishwa na tume hiyo ya ushindani alipozungumza na waandishi wa habari Oktoba 2020.

Mara baada ya tuhuma hizo mnamo tarehe 19 Novemba, 2020 tume hiyo ilitolea ufafanuzi kauli hiyo na kueleza kuwa, FCC haihusiki nan a kukwamisha mchakato huo bali wahusika ambao ni klabu ya Simba kuwa na mwitikio hafifu katika kuwasilisha nyaraka mbalimbali.

Toka siku hiyo tume hiyo iliamua kusimamisha mchakato na kufanya uchunguzi wa kwanini hawakuwasilisha taarifa ya muungano kati ya klabu ya Simba na Simba Sports Club Limited.

Mpaka sasa mfanyabiashara Mohammed Dewji ndio aliyeshinda zabuni ya ununuaji wa hisa asilimia 49 zenye thamani ya Sh. 20 bilioni, huku hisa asilimia 51 zikiunzwa kwa wanachama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

error: Content is protected !!