May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

FC Platinum yabariki usajili wa Chikwende Simba

Perfect Chikwende akisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Simba

Spread the love

KLABU ya FC Platinum inayoshiriku Ligi Kuu nchini Zimbabwe imethibitisha kuwa imefikia makuabaliano na Simba kuhusu uhamisho wa kiungo wao mshambuliani Perfect Chikwende. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Chikwende alionekana mwiba mara baada ya kuwafunga Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa nchini Zimbabwe kwenye mzunguko wa kwanza na kufanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na baadae kufungwa bao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya FC Platinum imeeleza kuwa timu zote mbili zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa mchezaji huyo na hivyo wanamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya.

Mchezaji huyo ambaye ameshatua nchini huenda akatambukishwa leo tarehe 15 Januari, 2021 kama mchezaji mpya wa klabu ya Simba.

error: Content is protected !!