Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Fatuma Karume: Naachia ngazi TLS
Habari za Siasa

Fatuma Karume: Naachia ngazi TLS

Fatuma Karume, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS)
Spread the love

FATUMA Karume, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) hatogombea tena nafasi hiyo baada ya kustaafu Aprili mwaka huu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Karume, mwanasheria huyo mwiba kwa Serikali ya Awamu ya Tano na mtoto wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Mstaafi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zabzibar ameeleza kuwa, nguvu kubwa baada ya kumaliza muhula wake wa mwaka mmoja ulioanzia Aprili mwaka jana, itakuwa ni kwenye biashara zao.

Katika orodha ya wanachama wa chama hicho waliojitosa kugombea nafasi hiyo, jina la Karume halikuwemo na alikuwa hajatoa maelezo yoyote.

Ikiwa leo ni tarehe 18 Februari 2019, zimebaki siku tatu kuhitimisha muda uliowekwa na kamati ya uchaguzi wa kuorodhesha majina ya wataowania nafasi hiyo. Kamati hiyo ilieleza mwisho kuwa tarehe 20 Februari 2019 (Jumatano wiki hii) saa 11 jioni.

“Baada ya kumaliza muda wangu wa mwaka mmoja, sitagombea tena. Naelekeza nguvu kwenye biashara zetu,” amesema Karume alipozungumza na mtandao huu na kuongeza;

“Jamaa zangu wamenishauri vizuri kuwa, niwekeze zaidi muda wangu kwenye biashara zetu.”

Karume ndio rais wa kwanza wa TLS mwanamke tangu kuanzishwa chama hicho mwaka 1954 kupitia Sheria ya Bunge ya mwaka 1954 (The Tanganyika Law Society Ordinance 1954).

Katika uchaguzi wa mwaka jana wa TLS, Karume ndiye mgombea aliyejitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi hiyo ambapo alimbwaga Godfrey Wasonga, Godwin Ngwilimi na Godwin Mwapongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!