Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Fatma Karume: Nimefukuzwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Fatma Karume: Nimefukuzwa

Fatma Karume
Spread the love

FATMA Karume, mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu nchini, amefukuzwa katika Kampuni ya Uanasheria ya IMMMA aliyoshiriki kuianzisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akieleza kufukuzwa kwake, Fatma ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya sasa, anahusisha tukio hilo na kile alichokiita ‘uovu’ unaotokana na harakati zake.

“Hii ni kuwajulisha nyote kwamba, nimefukuzwa kwenye ofisi niliyoijenga. Uovu wangu, uanaharakati,” ameandika Fatma kwe nye ukurasa wake wa twitter leo tarehe 21 Septemba 2020.

Mwanaharakati huyo ameuambia mtandao huu, kwamba kabla ya kampuni hiyo kumchukuliwa, ilimuandikia ya barua ya onyo ikimtaka kuacha mara moja shughuli za uanaharakati, na kwamba  asipofanya hivyo, angefukuzwa.

“Nafikiri kwa kuniondoa mie watapata kazi zaidi, kwa hiyo suala ni kwamba ni kunifukuza mimi ili wapate kazi nyingi,” amesema Fatma na kuongeza:

“Sababu kuu ya kunifukuza ni uanaharakati wangu, na waliniandikia kabisa kwenye barua kabla ya hatua hii, kwamba niache harakati zangu la sivyo watanifukuza.”

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa tarehe 16 Septemba 2020 na Sadock Magai, Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo, Fatma ameondolewa katika sehemu ya umiliki wa kampuni hiyo baada ya mkataba wake alioingia tarehe 26 Machi 2007 kuvunjwa.

Barua hiyo inaeleza kuwa, mkataba wa Fatma kuwa sehemu ya mmiliki katika kampuni ya IMMMA Advocate, umevunjwa tarehe 16 Septemba 2020, baada ya washirika wenzake kufika makubaliano ya kuvunja ushirikiano naye.

“Washirika wenzio walikutana tarehe 16 Septemba 2020, kujadili na kuamua kwamba hawataki tena kufanya biashara na wewe. Washirika wenzio wameamua kukuondoa kama sehemu ya mmiliki na kuvunja mkataba wako kuhusu maslahi yako yote katika kampuni,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Aidha, barua hiyo imemtaka Fatma kukabidhi ofisi ndani ya siku 30, tangu siku ya uamuzi huo kutolewa. “Ndani ya siku 30 tangu kutolewa kwa maamuzi haya, tunakuomba ukabidhi kila kitu ambacho kiko mikononi mwako,” inaeleza barua hiyo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!