Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Fatma Karume atoa somo la demokrasia, amkosoa Msajili
Habari za Siasa

Fatma Karume atoa somo la demokrasia, amkosoa Msajili

Spread the love

FATMA Karume, Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, ametoa somo la demokrasia kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, unaofanyika leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkutano huo wa ACT-Wazalendo unalenga kupitisha wagombea Urais wa Tanzania na Zanzibar wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba, 2020.

Bernard Membe ajitosa kuomba ridhaa ya ACT-Wazalendo kugombea Urais wa Tanzania huku Maalim Seif Sharif Hamad akitia nia kugombea Urais wa Zanzibar.

Fatma aliyealikwa kwenye mkutano huo, amewataka viongozi wa ACT-Wazalendo kuienzi demokrasia kwa kuuleza mfumo wa vyama vingi ulionaza mwaka 1992 na uchaguzi wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 unapaswa kuendelezwa

“Sisi kwenye historia yetu tumejaribu mfumo wa chama kimoja na tumeelewa kwamba huu ni mfumo ovu, mbovu na mbaya sana kwani ni mfumo wa zidumu fikra za mwenyekiti,” amesema Fatma

Aidha, Fatma amesema, mfumo wa vyama vingi unapaswa kulindwa kwa kuhakikisha vyombo vya utoaji haki na usalama vinakuwa hiru

“Mfumo unatakiwa kulindwa na tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, msajili huru na vikosi vya usalama huru. Uhuru unatokea kwenye mfumo,” amesema Fatma.

Fatma ametumia fursa hiyo, kukosoa kauli iliyokuwa imetolewa awali na Sisty Nyahozi, Msajili msaidizi wa Vyama vya Siasa aliyevitaka vyama vya siasa kufuata sheria.

Fatma amueleza Nyahozi kwamba sheria zinazokinzana na Katiba ya nchi sio halali.
Akizungumza katika mkutano huo, Nyahoza amevitaka vyama vya siasa kuhakikisha vinazingatia sheria za nchi.

Ulipowadia wasaha wa Fatma ambaye ni mtoto wa rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume amesema, “Leo hii kasimama Sisty anasema lazima tufuate sheria, kuna sheria mama ambayo ni Katiba, sheria zote nyingine zilizopitishwa kama zinakinzana na katiba sio sheria halali, hilo ni jambo Sisty aelewe.”

Fatma amesema, Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyopitishwa hivi karibuni inakinzana na Katiba ya nchi kwa kuwa Katiba inaeleza majukumu ya ofisi yake ni kusajili na si kulea vyama.

“Hata hiyo sheria aliyopitisha juzi ya ofisi yake ya msajili, eti yeye kafanywa mlezi wa vyama vya siasa. Kazi ya msajili ni kuweka rekodi za umma, kazi yake si kulea vyama vya siasa. Hakuna hiyo na ndio maana anaitwa msajili sio mlezi, ingekua kazi yake kulea angeitwa mlezi,” amesema Fatma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!