August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Farid kutimkia Hispania kesho

Farid Mussa (20) wa klabu ya Azam FC (Kulia)

Spread the love

HATIMAYE winga wa Azam Fc Farida Mussa, anatarajia kuondoka nchini kesho Juma tano majira ya Saa 5 kamili usiku na ndege ya Shirika la KLM, kwenda nchini Hispania kuanza maisha yake mapya ya soka, katika klabu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini humo, anaandika Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Farid ambaye alitakiwa aondoke mwisho wa msimu uliomalizika lakini ilikuwa ngumu kutokana na kutokamilisha baadhi ya taratibu zitakazo muwezesha kufanya kazi akiwa ndani ya nchi hiyo katika kipindi chote atakacho cheza soka akiwa Hispania.

Akitoa taarifa kamili juu ya kukamilika kwa safari ya mchezaji huyo, afisa habari wa klabu ya Azam Fc Jaffa Idd amesema kuwa faridi anaondoka baada ya Tenerife kumtumia tiketi ya ndege tayari kabisa kwenda kujiunga nao.

“Mchezaji Farid Mussa kama mnavyokumbuka tuliwaambia taratibu zake zinakwenda vizuri baada ya kukamilisha taratibu zote ubalozini, tunavyoongea na nyinyi hivi sasa ni kwamba klabu ya Tenerife imetuma tiketi ya Farid Mussa na anatarajia kuondoka kesho saa 5 usiku na ndege ya Shirika la KLM, atatoka Dar es Salaam, atapitia Amsterdam, Barcelona na baadaye Tenerife,” alisema.

Licha ya hayo msemaji huyo aliongezea ya kuwa Azam Fc inamtakia kila la kheri mchezaji huyo katika safari yake mpya ya maisha ya soka kwenye klabu hiyo ya nchini Hispania.

“Kwanza tunamtakia kila la kheri, acheze kwa mafanikio na kuonyesha uwezo mkubwa ili iwe ni sehemu ya kufungua milango kwa wachezaji wengine kutoka Azam FC au klabu nyingine yoyote ya Tanzania,” aliongezea Jaffar.

Ikumbukwe Farid anaondoka nchini kwenda  kujiunga na timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili kwa mkopo baada ya taratibu zote kukamilika za vibari na klabu ya Azam Fc kukubaliana na Tenerife juu ya masuala ya mikataba endapo watataka kumuuza mchezaji huyo kwenye klabu nyingine.

error: Content is protected !!