Monday , 29 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Familia zatengwa na kijiji cha Mureru
Habari Mchanganyiko

Familia zatengwa na kijiji cha Mureru

Spread the love

FAMILIA mbili za Kijiji cha Mureru, Kata ya Lalaji, wilayani Hanang’ zimedasi kuishi kwa kuhofia maisha yao baada ya kutengwa na jamii kijijini hapo kwa kosa la kuikatalia serikali ya kijiji kuchukua maeneo yao bila kuwashirikisha, anaandika Mwandishi Wetu.

Hata hivyo, serikali ya kijiji imesema kuwa watu hao ni wafamizi katika eneo la msitu wa Senga.

Taarifa za familia hizo kudaiwa kutengwa zilielezwa na Matayo Gileksa na Elia Karani mwishoni mwa wiki kijijini hapo wakati wakizungumza na Nipashe huku wakimtupia lawama mwenyekiti wa kijiji hicho kuongoza wananchi kuwatenga watu hao.

“Sisi kwa sasa tumetengwa na jamii hivyo hata tukitokewa na tatizo la kufiwa inabidi tuzike wenyewe na tumezuiliwa kunywesha mifugo yetu kijijini hapa ikitokea mtu akaongea na sisi naye anatengwa,’’ amesema Gileksa.

Aidha, amesema chanzo cha kutengwa ni baada ya kuwepo msuguano wa muda mrefu juu ya ardhi ambapo serikali ya kijiji iliwataka kuondoka maeneo wanakoishi bila kuwaonesha sehemu nyingine.

“Haya maeneo walikoamuru tuondoke ni maeneo ya urithi wa wazazi wetu waliotuachia lakini wameamua kutuondoa, na sisi hatuko tayari kwa kuwa hawajatushirikisha kwenye maamuzi ya kutupa fidia badala yake wanatulazimisha,’’ amesema.

Amesema watakubaliana na serikali ya kijiji endapo watawapa maeneo mengine yanayoendana na maeneo yao lakini siyo kuwaambia wawape ekari 15 wakati maeneo yao ni makubwa.

“Sisi tunaiomba serikali itume timu ya wataalamu waje hapa wapime maeneo yetu alafu ndio sasa tupelekwe maeneo yanayostahiki siyo kutunyanyasa na kututenga ili tukubaliane nao,’’ alieleza

Kwa upande wake, Elia Karani, alisema kufuatia jamii kuwatenga anaishi kwa mashaka hata akilala usiku hawana uhakika na usalama wao kwa kuwa jamii ya kule ikishasema kitu ni lazima itekeleze ndio maana wanaishi kwa wasiwasi.

Lakini alisema anashangazwa na serikali ya kijiji hicho kuwatimua kwenye maeneo yao na kutaka kuwapeleka maeneo ya malisho ambapo bado watakuwa kwenye matatizo.

Ameomba serikali ya wilaya na taasisi za haki za binadamu kuwanusuru katika kadhia hiyo inayoweza kuwasababishia matatizo makubwa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, James Kejalu, alipoulizwa na Nipashe kwa njia ya simu alikiri kuufahamu mgogoro huo ila akadai kuwa watu hao walikuwa ni wavamizi ambao ni jamii ya wafugaji.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Sara Msafiri, amesema haujui mgogoro huo licha ya watu hao kuwa na nakala za malalamiko yao kutoka ofisini kwake na akadai kama walifika na hawakuridhika warudi tena ofisini kwake atawasikiliza.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Daud Arajika, alikiri kuufahamu mgogoro huo hivyo akasema wako mbioni kuitisha kikao cha serikali ya kijiji ili kuzungumzia mgogoro huo ila suala la kutengwa alisema halijui.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

Habari Mchanganyiko

Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa

Spread the love  KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imezinduliwa...

Habari Mchanganyiko

NMB ya kwanza kuzindua Malipo kwa QR na UnionPay International

Spread the loveBENKI ya NMB kwa kushirikiana na UnionPay International (UPI), wamezindua...

error: Content is protected !!