Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Familia ya Lissu yaibuka na kuing’ang’ania serikali
Habari za SiasaTangulizi

Familia ya Lissu yaibuka na kuing’ang’ania serikali

Alute Mughwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Vincent Mughwai
Spread the love

FAMILIA ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu imeibuka na kuing’ang’ania serikali ikitaka uchunguzi wa kina ufanyike ukihusisha wachunguzi wa nje ili kubaini watu waliomshambulia ndugu yao kwa risasi mkoani Dodoma, anaandika Fakis Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari, kaka mkubwa wa Lissu, Alute Mughwai Lissu, kwa niaba ya familia amepaza sauti na kuhoji ni kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama havijawapata watu waliohusika kumshambulia ndugu yao.

Lissu alishambuliwa na watu ambao hawajajulikana mpaka sasa na kupigwa risasi zaidi ya risasi 38 zilizomsababishia majeraha katika mwili wake na kukimbizwa hospitali nchini Kenya.

Tukio hilo la kinyama lilitokea mjini Dodoma, Septemba 7, mwaka huu na kukimbizwa hospitali ya mkoa huo kabla ya kuhamishiwa siku hiyo hiyo nchini Kenya ambako hadi sasa bado anapatiwa matibabu.

Mughwai amesema familia hiyo imemuandikia barua mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju kuhusu tukio hilo la ndugu yao kushambuliwa na watu wasiojukana.

Alitoa mfano kwamba hivi karibuni alishambuliwa mwanajeshi mstaafu na uchunguzi wake ulifanyika haraka na watuhumiwa wamekamatwa.

“Ni vyema uchunguzi ufanyike kama inavyofanyika katika matukio mengine ambayo yametokea hapa nchini” amesema Mughwai.

Amesema kuwa kuchelewa kwa uchunguzi kunaleta wasiwasi kwa kuwa mpaka sasa hakuna mtu yoyote aliyekamata kuhusiana na tukio hilo ambalo siyo rafiki katika jamii yoyote.

Amefafanua kuwa kusimama kwa uchunguzi bila kuwa na sababu ya msingi siyo jambo jema kwani unapaswa kuendelea na watu waliohusika wakamatwe.

“Kama dereva wa Tundu Lissu anahusika katika uchunguzi vyombo vya dola vinatakiwa kwenda kumfuata na kumhoji kama wanavyofanya katika matukio mengine” amesema Munghwai.

Amesema kwamba serikali imekuwa ikitumia wachunguzi kutoka mataifa mengine ili kuongeza nguvu katika kuwakamata wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya dola.

Ametoa mfano kuwa mwaka 1998, Ubalozi wa Marekani nchini ulipolipuliwa serikali ya Tanzania ilishirikiana na wachunguzi wa FBI na kufanikiwa kuwabaini wahusika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!