FAMILIA ya Mfanyabiashara, Mohammed Dewji ‘MO’ aliyetekwa tangu Alhamisi ya Oktoka 11 2018, maeneo ya Osterbay jijini Dar es Salaam, imetangaza zawadi nono ya kiasi cha Sh. 1 bilioni, kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Zawadi hiyo imetangazwa leo tarehe 15 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Familia ya Gullam Dewji, Azim Dewji wakati akizungumza na wanahabari.
“Familia ya Mzee Gulam inasikitika kutangaza kutekwa kwa mtoto wao mpendwa MO, mtendaji mkuu wa METL. Aidha, tunapenda kuishukuru serikali kwa jitihada kubwa wanazofanya kuhakikisha tunampata mtoto wetu, vile vile tunavishukuru vyombo vya habariokwa kazi kubwa, taasisi za dini na zisizo za dini kwa maombi na kutufariji katika kipindi hiki tunaomba muendelee,” amesema.
“Katika kuongeza juhudi za kuhakikisha mtoto wetu mpendwa anapatikana, familia inapenda kutangaza zwadi nono ya fedha za kitanzania bilioni 1 kwa yeyote atakayetoa taarifa muhimu zitakazopelekea kupatikana kwa Mo,” amesema msemaji huyo wa familia ya Dewji.
Azzim ameeleza kuwa, familia hiyo itatunza siri za mtu atakaye toa taarifa za kupatikana kwa Mo Dewji, huku akitaja mawasiliano ya familia hiyo kwa mtu atakayetaka kutoa taarifa.
“Familia inaahidi kutunza taarifa kwa siri kubwa ya mtoa taarifa. Kwa yeyote mwenye taarifa aitoe kwenye namba 0755030014, au 0717208478 na 0784783228,” amesema Azim.
Leave a comment